HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

19 July 2013

KWA HILI MICHAEL RICHARD WAMBURA UMENENA NAUNGA MKONO HOJA



 
Habari msomaji  wangu leo nilikuwa na tazama kituo cha runinga cha StarTv katika Kipindi cha  tuongee Asubuhi leo  walikuwa wamewaalika Msemaji wa shirikisho la soka la Tanzania Tff Boniphase Wambura Mgoyo  na aliyekuwa Katibu mkuu wa chama hicho zamani FAT na baadae Tff Michael Richard Wambura.

 Bila shaka kwa majina haya  niliyokutajia wote hawa watakuwa wenyeji wa Mkoa wa Mara mkoa ambao unasifika zaidi kwa kutumia nguvu nyingi akili kidogo hasa kwa` wakazi wa mkoa huo lakini hawa hawako hivyo  wawili hawa hutumia akili nyingi kujadiri mambo kwa hoja.

Naanza na  Michael Wambura kiukweli moja kati ya watu ambao wanaweza kuchukiwa na kuonekana wa baya katika soka la Tanzania ni Wambura ambaye kila utakaposkia kuna chaguzi yoyote inataka kufanyika hasa katika wakati wa pingamizi na yeye lazima pingamizi lake litakuwemo Eidha mtu anasifa au kukosewa kwa kanuni au sheria au badiliko lolote la kikatiba la tff  au chama chochote cha soka.

Hapo ndipo hukera watu wengine ambao wanamtazamo tofauti na yeye katika swala zima la kanuni lakini wakati natazama kipindi kile Tom chilala mtangazaji wa kipindi hicho ambaye alikuwa akisimamia kipindi kwa upande wa Dar Es –Salaam alimuuliza swali Michael Wambura kuhusu Udhamini wa michezo Mbalimbali katika soka la Tanzania  bila kujari  ligi au  mashindano ya vijana .

Wambura akaanza kujibu Kwanza alinijibu swali ambalo siku yoyote kama ningekutana na watu wa  TBL ningewauliza lakini yeye akanijibu kisomi zaidi alianza kunibadili kimtazamo sana kwa kusema TBL haina makosa kudhamini Timu ya soka taifa ya Tanzania yaani taifa stars kwa sababu ndiko mahala pake licha kuwa inatumia pesa nyingi kwenye timu ambayo haina tija .
 
Akasema TBL haiwezi kudhamini timu za vijana kwa sababu kisheria hairusiwi kufanya hivyo kwa sababu hata pombe yenyewe watoto hawarusiwi kunywa sembuse kudhamini  wambura akaendelea kusema hata hizo kampuni zinzodhamini  michuano ya watoto ambayo TBL inashindwa haifanyi hivyo kwa kiwango stahili akatoa mfano kuwa Baadhi ya kampuni moja ambayo hudhamini mashindano ya hayo  inatoa shilingi laki mbili kundesha ligi ya za michuano hiyo kwa vijana kitu ambacho kwa mikoani si pesa kabisa hasa katika soka la Tanzania kwani hata pesa kwa Dar Es salaam kwa pesa hiyo hata kwa nauli haitoshi bado  kunatakiwa kutazamwa upya katika swala la udhamini .


Nilivutiwa sana na wambura kwani ukitazama kwa pesa aliyoitaja sipesa ya kundeshea programe za vijana tena akaweka na msisitizo  kuwa mashindano hayo ambayo huchezwa mara moja kwa mwaka kiukweli kwa alichokizungumza wambura ni tofauti na vile nilivyokuwa nikimfikiria siku zote  hapa aliongea kisoka zaidi tena kwa jicho la mbali hata mimi namuunga mkono Michael wambura ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa simba yakati fulani  kwakweli vile nilivyokuwa nikimtazama na kumchambua sasa imekuwa tofauti kidogo alinikuna kwa kuongea mambo ya msingi katika soka .

Wambura akaulizwa tena na Tom mwana wa Chilala kuhusu mustakbari wa soka la Tanzania na matarajio ya timu ya soka ya taifa kuhusu mashindano ya kombe la CHAN mashindano yanahusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani
Wambura anasema kuwa shida ya Tanzania huwa inataka kuonekana ipo wakati mipango ya soka haipo  anasema kuwa ukitazama vizuri mechi ya Tanzania na Uganda ya kwenda Chan ,tayari Uganda inanafasi kubwa zaidi kwani ukitazama kwa upande mwingine timu yoyote ile Duniani inapokwenda kucheza Ugenini huwa inajaribu kufanikisha mambo yafautayo Eidha kutoa suluhu au kutoruhusu magoli mengi ya kufungwa lakini wao Uganda walishatufunga hapa kwetu kwake yeye tayari mechi ishakwisha kwani itakuwa ngumu kushinda mechi na Uganda katika uwanja  wao.

Ila akasema kitu pekee kitakachoweza kuifanya Tanzania kushinda mechi hiyo ni kuweka akili yao katika soka ya kisomi  yaani professionalism akiwa na maana ya bila kujari idadi ya mashabiki wa uganda watakuwa wangapi kiwanjani, wao wanachotakiwa kujari ni kwamba mashabiki hao hawachezi wanaocheza ni wachezaji  ndio maana hata tembo wa ivory coast walitufunga kwa sababu wao walifanya kama alichosema
Kama kawaida ya wambura hakuacha kuponda michuano hiyo ambayo watanzania wengi ndiyo imebaki kuwa tumaini lao lakini akasema ya kuwa`mashindano hayo nchi nyingi zilizo endelea zimekuwa zikichukua wachezaji wa majaribio japokuwa nao huwa sio wa kulipwa ndio maana nchi kubwa kisoka za afrika hazitilii maanani michuano hiyo kwa sababu kubwa kuwa haitambuliki na fifa kwa hiyo hata wasipo shiriki haiathiri jambo lolote hapa ukitazama wambura anakuja na hoja ya msingi kidogo.

Lakini ukitazama ni kama anaipiga kijemmbe shirikisho la soka la Afrika CAF wambura akajibu swali jingine kuhusu tiba ya michezo sehemu ambayo kwa afrika ni jambo ambalo halitiliwi mkazo sana kwasababu ya kutopewa kipaumbele hasa na wachezaji kuumia na kutopewa tathimini ya kutosha matokeo yake huishiwa kupigwa Ganzi kila uchao na kufika kipindi majeraha kukithiri mwilini na hivyo kujikuta mchezaji akiwa na umri mdogo kukimbilia kucheza veteran anasema ukitazama waganga wanaotibu wachezaji katika timu husika hawazidi nane kitaaluma  wakati mwingine mganga huyo huyo mmoja kuajiriwa mara mbili klabuni na timu ya taifa sasa je Timu za mikoani wako wangapi ?
Aliniacha hoi bin Taaban kwa yake aliyoyasema kwani alizungumza ukweli mtupu kuhusu jambo hilo nilipunguza hasira zangu kwa yale aliyofanya nyuma kimtazamamo na inawezekana kuwa Wambura anazungumza mambo ya kimsingi lakini na yeye ni mwandamu anaweza kuwa na mapungufu yake ndo maana amebarikiwa kuweka pingamizi si ajabu anaweza kufanikiwa mara baada ya katiba ya tff  kubadilishwa au kufanyiwa marekebisho maana sisi wengine sio watalaamu kisheria japokuwa yanaweza ya kamkuta tena kwani hizo kamati zitafuata kanuni zile zile ambazo mwanzo zilikuwa zikimtoa nishai .
                                                           
Namaliza na msemaji wa shirikisho ambaye yeye aliyongumza  kuhusiana na timu na mandalizi na maendeleo ya kambi ya timu ya taifa japokuwa kuna wakati Abdallah Tilata alimchokoza kwa kumuuliza vp kuhusu Athumani Iddy kuikacha timu ya taifa na baadae anaonekana kufanya mazoezi na timu mwanza tena kwa hari ya juu Waambura anasema kuwa Athumani iddy bado yupo timu ya taifa na muda ukifika pale atakapoona inafaa ataandika barua ya kustaafu timu ya taifa ili aongeze`nguvu timu yake anayochezea klabuni.  

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers