HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

29 August 2013

MANJI APELEKA MASHINDANO YA BASKELI DODOMA
 
Mashindano ya taifa ya mchezo wa Baskeli  yatafanyika mkoani Dodoma Mwezi Ujao. Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Baskeli Nchini   Tanzania (CHABATA) Nazil Manji Ametanabaisha hayo jana .
Manji amesema Baraza la michezo limekubaliana na chama chake kuwa mashindano hayo yafanyike Tarehe 29 Mwezi kenda Mkoani Dodoma.
CHABATA imekusanya pesa lakini ilikuwa ikisubiri Baraza la michezo kupanga Tarehe ya mashindano na sasa`wanafuraha kwani wanafanya jambo amabalo walishindwa kwa miaka mingi .
Manji anaongeza kuwa  CHABATA ilitaka kuandaa pamoja na Tarehe ya Uchaguzi mkuu lakini wanasubiri Tarehe itakayopangwa na  Baraza la michezo .
Manji amesema kuwa hawana pesa za kutosha za kufanya mambo yote mawili kwa wakati mmoja na kama kawaida ya vyama vingine naye ameomba msaada kwa makamapuni kuisadia  CHABATA kutimiza lengo hilo. Baada ya mashindano hayo Chabata itakaa na kujadiri maendeleo ya mchezo huo.

Amesema kuwa jumla ya waendesha baskeli 100 wanatarajia kushiriki mashindano hayo ambayo yatafanyika katika ngazi ya kimataifa .

ambapo wanatarajia kuyafanya katika ngazi ili kuwaongezea washiriki uwezo na uzoefu .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers