HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

18 November 2013

BAUSI AWEKA HADHARANI 21 CHALENJI CUP

 
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa Zanzibar ‘Zanzibar Heroes Salum Nassor Bausi ametangaza majina ya wachezaji 21 watakaoshiriki michuano ya Chalenji Novemba 27 mwaka huu, nchini Kenya.
Zanzibar Heroes ambayo imepangwa kundi moja na wenyeji wa michuano hiyo inatarajiwa kuondoka nchini Novemba 24 mwaka huu.
Akitaja majina hayo kwa niaba ya kocha huyo Kocha wa Makipa Saleh Machupa amesema kuwa kabla ya kuondoka watafanya mchujo wa mchezaji mmoja ili kupata idadi ya wachezaji 20 watakaokwenda nchini huko.
Alisema kuwa kikosi hicho awali kilikuwa na wachezaji 25 ambapo wanne wameachwa huku Mwadini Ali wa Azam na Mohammed Juma wa timu ya Polisi wakiachwa kwa kuwa na maumivu ya mguu.

Wachezaji hao waliotajwa ni Salum Kassim, Suleiman Kassim Serembe, Shafi Hassan, Amour Omar Janja, Khamis Mcha, Waziri Seif, Abdallah Rashid na Mohammed Faki.
Wengine ni Salum Khamis, Hamad Mshamata, Said Yussuf, Suleiman Ali, Amiri Hamad, Ali Badru, Masoud Ali, Awadhi Juma, Adeyoum Saleh,  Mohammed Othman na Seif Rashid Karihe.
Kikosi hicho kipo kambini kwa muda wa wiki moja sasa na kinaendelea vizuri na mazoezi ambapo hufanya mazoezi yake katika uwanja wa Mao Tse Tung, na kutarajiwa kucheza mechi saba za kirafiki kabla ya kuondoka kwake

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers