HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

5 November 2013

HIKI NDICHO KINACHOWAKWAMISHA WACHEZAJI WA TANZANIA KUSHINDWA KUCHEZA SOKA YA KULIPWA AFRIKA ,ASIA NA ULAYA
Moja kati ya Mambo mengi yanayowakwamisha wachezaji hasa wa Tanzania kucheza soka Ulaya ni uelewa wa mambo ya kimsingi katika Soka hasa la kisasa . Wapo wachezaji wengi kutoka Tanzania ambao wamewahi kwenda hata Uingereza kujaribu kucheza na kuishia patupu lakini jambo la muhimu na La msingi ni kutafuta sababu kwanini wanashindwa kucheza soka ulaya .

Wengi wetu tunawajua baadhi ya wachezaji walioweza kwenda kujaribu kucheza soka ulaya wengine wakichukuliwa na timu zinakuja kufanya Ziara katika vipindi vya mapumziko na kupata nafasi ya kuchukuliwa kwenda huko lakini sitaki kuwataja majina wachezaji hao na ninakwenda kwenye Alama ya msingi .

Lugha-:  wachezaji wengi wakiTanzania  hawajui Lugha kitu kinachowapa tabu saba makocha wanaozungumza na huko majuu hiki ni kitu cha msingi bila Lugha huwezi kucheza soka ulaya zipo lugha kuu Tano za soka Duniani Kiingereza,Kijerumani,Kitaliano,Kiispaniola ,Kireno  na Kifaransa ambapo lazima mchezaji huzungumze Lugha moja kati ya Hizi lakini kwa Tanzania ni wachezaji wachache sana ambao wanatilia umaanani wa Kuzungumza Hasa ya kiingereza ambayo ndiyo Lugha ya kurithi kwa mkoloni mwingireza  lakini wameishia kuchemka wengine hata Lugha zao za asili za makabila hawazijui .

Wachezaji wengi kutoka afrika wanaozungumza baadhi ya Lugha Tajwa hapo wengi wanacheza soka ya kulipwa ulaya ni Rahisi kufundishika kwa lugha husika.

Elimu -: hili ni tatizo jingine Tena la msingi kwani   wachezaji wengi hasa wa Tanzania huishia Darasa la Saba ambalo kwa sasa silolote sio chochote kwani baadhi ya wanafunzi wanashindwa kuandika hata majina yao wenyewe sasa  mchezaji kama akifika ulaya atawezaje kuelewa anachofundishwa tena hapa ndipo kwenye msingi mkubwa ambao watanzania wengi wanachemsha kwa sababu utapimwa hata uelewa wako Darasani sasa kocha wa mpira wa Miguu na mwalimu wa kawaida wa Darasani hawana Tofauti wanataka mwanafunzi aelewe anaposhindwa  kuelewa hatoweza kucheza mpira.

Tamaa za klabu -: klabu ambazo zinawamiliki wachezaji wanaoonekana kucheza vizuri katika soka ya kitaifa ambao wengi hupambwa hata na Magazeti kupitiliza na kuanza kufananishwa na wachezaji wakubwa Dunia huzitia jeuri klabu na kutaka kudai pesa nyingi kwa wachezaji ambao hawana viwango kwani wachezaji wengi watanzania huwawanafikili kuwa wanauwezo wa kucheza ligi kuu ya za mbaliambali za Ulaya wakati kuna baadhi ya wachezaji huko ulaya wamewazidi uwezo na wanakaa nje ,Klabu zinapotaka pesa nyingi ni kutaka kuwanyima wachezaji hao fusra ya kutaka kucheza soka ulaya na Asia.

Ulevi na starehe -: Hakika hapa ndipo wachezaji wengi kutoka Tanzania wanapomaliza soka kwani hutawakuta kwa wingi katika klabu za usiku wakinywa na kuchukua wanawake kwa umaarufu wa magazeti na soka yao butu na wengine hushinda kwenye kurasa za Kui saa ishinrini na nne wakichat na wanawake na kusahau mafunzo kiwanjani na hapo ndipo soka yao inapokwenda Kaburini ni aibu kwa mchezaji kutoka Tanzania kutocheza hata robo fainali ya kombe la afrika kwa vilabu ni fedheha kabisa  ,ulevi na starehe huwanya wachezaji kuwa wavivu na kuzembea mazoezi na kuuwa vipaji vya soka.

Jambo jingine Japokuwa sio la kuliombea kwa Tanzania nchi yetu haijawahi kupatwa na shida kama Vita,Mafuriko,kukosa chakula kuliko kithiri ndio maana tunapata kizazi ambacho kinafikili kuwa mambo hushuka kama maandiko ya viatbu vitakatifu kuwa vitakuwa kwa miujiza na kuondoa jkt ndio kimekuwa chanzo cha kupata kizazi kilichoshindikana kwa maadili na kupata wachezaji wabaovu wasio kuwa na nidhamu huko kumewafanya wachezaji wa kitazanzania kuchemka kujituma kiwanjani na kuleta visingizio vingi .


La mwisho kabisa wachezaji wetu wa kitanzania hawajitambua kwa kila kitu na kutoka kuwa na Miundo mbinu ya soka na baadhi ya timu mpaka zinaingia katika Karne ya 21 hata kiwanja Binafsi cha mazoezi hawana je unaweza kuendesha soka kwa utaratibu huuuu? 
 
 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers