HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

23 December 2013

BRANDTS YAMKUTA YA KIBADENI YANGA
Bin Kleb (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu leo Jangwani. Wengine kulia ni Ofisa Habari, Baraka Kizuguto na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Mussa Katabaro 


Bin Kleb amesema sababu za kumuondoa kocha huyo ni kushuka kwa kiwango cha timu katika siku za karibuni na haijatokana na kipigo cha juzi pekee. “Kweli mwanzoni alipandisha kiwango cha timu, kilipanda sana, lakini baadaye kiwango kikaanza kushuka, tukasema tumpe muda kidogo, lakini tunaona mambo yanazidi kuharibika, Bin Kleb amesema sababu za kumuondoa kocha huyo ni kushuka kwa kiwango cha timu katika siku za karibuni na haijatokana na kipigo cha juzi pekee.
“Kweli mwanzoni alipandisha kiwango cha timu, kilipanda sana, lakini baadaye kiwango kikaanza kushuka, tukasema tumpe muda kidogo, lakini tunaona mambo yanazidi kuharibika, hivyo tumeamua kuachana naye,”alisema.
Kuhusu Wajumbe wengine wa benchi la Ufundi, Bin Kleb alisema kwamba taratibu nyingine zinafuata na wakati huo huo klabu inasaka mwalimu mwingine atakayerithi mikoba ya Brandts.


Aidha, Bin Kleb amethibitisha ushiriki wa Yanga katika Kombe la Mapinduzi Januari mwakani visiwani Zanzibar na pia timu itafanya ziara ya Ulaya baada ya michuano hiyo.  
Pamoja na hayo, Bin Kleb amesema hawezi kuwapongeza watani wao Simba SC kwa kuwafunga 3-1, kwa sababu siku hiyo Yanga ilicheza mpira mbovu na ingeweza kufungwa hata timu inayoshuka daraja. 
Binzubery story 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers