HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

2 December 2013

NINGEKUWA KOCHA WA KIGENI NISINGEKUJA KUFUNDISHA SOKA TANZANIA



Moja kati ya Jambo kubwa katika soka la Tanzania ukiwa kama kocha unalazimika kushinda mechi iliyopo mbele yako .


Tena ni mtazamo uliojengeka katika vilabu viwili vya kihistoria Simba na Yanga kwa  hakika ni vilabu vyenye ngome imara ambazo zinatumika visivyo.  Wengi wa wanachama na viongozi wa vilabu hufanya vitu kutokana na matakwa yao Binafsi simba na yanga ndio vilabu ambavyo vimefundishwa na makocha wengi zaidi wakiwemo wazawa na wageni :-  Katika kichwa changu cha habari cha msingi nimeandika ningekuwa kuwa kocha wa Kigeni nisinge kuja kufundisha mpira Tanzania tena naongeza hata kama ningekuwa Napata mshahara anaopata Gareth Bale achana na  wa Cristiano Ronaldo !


Lakini kwanini Nisingekuja kufundisha mpira Tanzania ? hili ndilo swali muhimu na ndilo linalo hitaji majibu hapa sitataja makocha  wengi lakini nitataja japo kwa kiupekee  Naaam naanza kutoa sababu lakini zaweza kuwa sio za msingi kwa upande wako hivi karibuni klabu za Simba na Azam zilisitisha mikataba ya makocha wao kwa kile wanachoamini kuwa hawajafanya yale wanayotaka hadi kufika sasa yawezekana ikawa kweli au uongo.


Sasa tuanze na simba ambao wao walimuondoa mfaransa Patrick Liewing na kumpa Abdallah Kibadeni kuifundisha timu ya simba mpaka nusu msimu simba imeshika nafasi ya nne na baadhi ya mashabiki na wanachama wakaanza kusema kuwa Kibadeni hafai kuifundisha simba jambo ambalo haliniingiii akilini kabisa nafasi nne unasemaje Kibadeni hajui kufundisha wakati anafundisha timu hiyo kwa mara ya kwanza , Kibadeni kabla hajaja simba alikuwa akiifundisha Kagera sugar ya Mkoa Kagera timu ambayo ilikuwa ikitishia usalama wa baadhi ya timu hasa simba yanga ,Mtibwa na Azam apa ndipo alipoonekana Lulu na klabu ya simba kumpa kazi lakini leo hafai .


Katika makocha wa Kigeni waliokuja kufundisha mpira Tanzania hakuna kocha hata mmoja aliweza kukaa zaidi ya Miaka miwili zaidi ya Stewart John Hall wa Azam japo hata yeye aliwahi kufungishwa vilago ambaye hivi karibuni alifungishwa vilago na klabu hiyo.


Hapa nilikuwa nakupa mwangaza tu sasa tuje kwenye sababu kuuu  kwanini Nisingefundisha Tanzania

Baada ya kocha wa Azam kuachia ngazi alipata kuhojiwa na moja kati ya  Televisheni moja nchini siitaji jina alisema haya baada ya kuuliza swali je unafikiri kwanini umeshindwa kutwaa ubingwa wa Tanzania.


Stewart alijibu hivi:-Sijashindwa  Simba na yanga wapo hapa Tangu siku nyingi sana kabla hujafanya chochote lazima ufanye utafiti kwanini hawa wanabadilishana wao Ubingwa tu niligundua yafuatayo katika miaka yote hakuna siku simba na yanga zimekuwa Katika kiwango Bora zote kwapa pamoja lazima Mmoja atakuwa juu mmoja atakuwa chini sasa la msingi jaribu kuwa katikati  yao kitu ambacho amefanikiwa kwa asilimia tisini na lililobaki ni kuutwaa ubingwa ambao pia hautwaliwi kirahisi hata kidogo.


Sasa ukitazama mazungumzo ya Stewart karibu sasa utaanza kupata majibu ya kwanini nisingekuja kufundisha soka Tanzania jambo kuu kuliko yote ni kuwa Vilabu Vingi vya Tanzania vimekuwa hazina mipango ya muda mrefu wao hutaka kushinda mechi iliyopo mbele yao hata kama hawawezi kushinda mechi hiyo.


 kifupi  kanuni za kufundisha simba na yanga unatakiwa kushinda tuu Epuka kutoa Suluhu au kufungwa  Tena simba au yanga mashabiki siku zote huwa hawapendi kufungwa lakini wa simba na yanga wamezidi  wao kufungwa kwao ni dhambi ukiwa kama  kocha hili haliwezekaniki hakuna timu isiyofungwa Duniani lakini ukiwa kocha wa kigeni hakikisha Hufungwi.


Jambo la pili katitika tawara  kuna kitu kinaitwa Bodi ya menejimenti au Tawara klabu za simba na yanga ni klabu ambazo kama zimelaaniwa hivi kiutendaji hakuna siku hata moja utakosa migogoro isiyokwisha kama viongozi hawawezi kuelewana na kupanga mambo yakapangika timu haiwezi kwenda na mtaishia kufungwa kila siku kwani uongozi wa vilabu hivi hauna tofauti na vijiwe vya kuvutia Mihadarati wakati mwingine fujo na maelewano yasiyokwisha makundi yanayotaka na yasiyotaka Baadhi ya viongozi wenye misimamo tofauti.


Mishahara ya makocha hapa unaweza kulimbikiziwa mishahara yako mingi na unaweza kujiuliza hawa pesa zao huwa wanapeleka wapi na kila siku unaskia vilabu hivi uongozwa na matajiri je matajiri hawa wanafanya biashara gani ukiacha hayo yooote unafikiri kwanini simba na yanga mpaka leo zimeshindwa kufanya Vizuri mashindano ya kimataifa hii yote ni kwasababu ya kubadilisha makocha kama shati .



Siku zote huwa nasema kuwa ili tufanikiwe katika soka yetu jambo la kwanza vilabu vya Tanzania vinatakiwa kubadili utaratibu wa kiuendeshaji tofauti na uliopo sasa Rais wa tff Jamali Malinzi  huwa anasema kuwa atanaka kutengeneza timu ya taifa ya chini nya miaka kumi na tano kwa maana ya Under 12 ilikifika miaka kumi na saba tushiriki michuano ya afrika kwa sasa nionacho ni kazi bure Tanzania haiitaji hayo  kwa sasa Shirikisho linahitaji kuunda utaratibu wa kuvisimamia vilabu vinavyoongozwa na kuendeshwa kwa kutumuia wanachama ,kusimamia miundo mbinu ya kisoka ,Elimu ya soka kwa wachezaji ,vilabu ambavyo vinaendeshwa kwa mfumo wa hisa wa kampuni haina haja ya kuvisimamia kwa sababu zinajiendeshea kimpango wake .


Ukiwa kama kocha kabla hujakwenda kwenye nchi husika lazima ujue tabia ya wachezaji ,Viongozi,Mashabiki wanchi unayokwenda Sidhani kama hawa makocha wanafanya utafiti wangekuwa wanafanya utafiti wasingekuwa wanakuja kufundisha Tanzania kwa sababu ya utaratibu mmmbovu wa kiutawala na miundo mbinu.

Kwa sasa Tanzania kuna makocha watano wa Kigeni lakini hakuna hata kocha hata mmoja wa Tanzania ambaye anafundisha Nchi moja ya Afrika mashariki na kati je unafikiri ni kwanini ?



Hapa tunaweza sema kuwa hatuna makocha wenye Elimu ya kufundisha au ndio tuseme kuwa Tanzania tunalazimisha mchezo tulioshindwa kucheza na kama tumeshindwa tufanye nini?



Shida moja kubwa ni kuwa kila kiuongozi wa soka anataka afanye mabadiliko kwa hatua kubwa hata kama hana muda wa kufanya hivyo kwa sasa soka ya Tanzania inavyofanya ni kama mtu anayejaribu kwenda Sherehe akiwa amevali suti huku kaoga Passport size, kapiga mswaki lakini hajachana nywele,hajavaa tai rangi ya koti na salawili tofauti kashika simu lakini haina salio la kutosha anapanda piki piki ambayo mwendeshaji hana Leseni huku element wote wakiwa hawana boda boda haina mafuta na sheli ni mbali kwa utaratibu huu hata Sudan ya kusini ,Somalia,Eritrea zikitulia na kuacha kipigana  zitatupita.


Ni dhahiri hatujielewi kwa hiyo nisingeweza kuja kufundisha soka Tanzania Nchi ambayo hata Vyombo vya habari vinachangia kuharibu soka lake kwani vinapenda kukuza migogoro isiyokuwa na msingi kuandika habari kishabiki  kujaza wachezaji sifa ambazo hawana kwani mfumo huuu Tanzania haita weza kufanikiwa kisoka mpaka Yesu au nabii Isah atakaporea Tena.

Hizi ndizo sababu ambazo zingenifanya nisje kufundisha soka Tanzania.        

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers