HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

11 May 2013

SOKA HAINA ADABU JAMANI SOMA HAPA


Ben Watson scores for Wigan against Manchester City in the FA Cup final

Wigan Athletic imeshinda taji baada ya miaka  81-katika historia ya klabu hiyo baada Ben Watson's kufunga katika dakika za mwisho katika fainali iliyofanyika katika uwanja wa  Wembley kwenye kombe la FA Cup dhidi ya machester city 
Roberto Martinez's amekuwa mhispania wa kwanza kutwaa taji katika ardhi ya uingereza huku akiiwezsha kwa mara ya kwanza timu ya ligi ya uingereza kuchukua ubingwa wa FA cup huku ikiwa katika hatari ya kushuka daraja  Pablo Zabaleta alilimwa kadi nyekundu kabla ya mchezo kumalizika na zilikuwa zimbaki dakika sita tu mpira kumalzika .
  akitokea kwenye Benchi Watson, ambaye amekosa msimu huu baada ya kuumia mguu mwezi November, Ndiye aliye wainua mashabiki wa Wigan's akiunganisha kichwa baada kupigwa  kona ya Shaun Maloney's na kuwafanya city kutoka bila kombe lolote msimu huu
.
 FA CUP KATIKA PICHA
 Kocha wa wigan Roberto Martinez akishangilia kombe na  Ben Watson's ambaye ndiye mfungaji wa goli pekee katika mechi hiyo.Manchester City defender Pablo Zabaleta is sent off in the FA Cup final
Mwamuzi wa mchezo wa kombe la FA CUP andy Marriner akimpa kadi nyekundu Pablo Zabaleta baada ya kumchezea faulo  Macmanaman

Wigan owner Dave Whelan Kissing mwah

MKASA WA Judith Wambura ( Lady JayDee) WAFIKA PABAYA SASA !!!

 Na Andrew Chale 0719 07 63 76
MWANAMUZIKI nguli wa bongo na kiongozi wa yenye mvuto nchini bendi ya ‘Machozi’,  Judith Wambura ( Lady JayDee) au  Jide ama #Teamaanaconda#,  anatarajia kuripoti Mahakama ya Kinondoni siku ya Jumatatu Mei 13, kufuatia kufikishiwa kwa taarifa hizo Gadna G Habash ‘Captain’ ambaye ni Meneja na mumwe wa Lady Jay Dee.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mchana wa leo, Gadna alisema ni kweli wamepata taarifa za kutaarifiwa kwa Lady Jay Dee kufika Mahakama ya Kinondoni, siku ya Jumatatu.
“Ni kweli tumepata wito na Mahakama ya Kinondoni,  Hii ni kufuatia kwa jana  kufika watu ambao walijielezea kuwa wanatoka Mahakama hiyo na walikuja na barua ya kumkabidhi Lady Jay Dee mwenyewe hata hivyo hawakumkuta” alisema Gadna.
Aliendelea kueleza kuwa, hata alipowaeleza watu hao wamkabidhi yeye hiyo barua watu hao walisema ilikuwa si lahisi zaidi alitakiwa akabidhiwe mlengwa, hivyo kumueleza kuwa wito wa kufika mahakamani siku ya Jumatatu, na  aliwakubalia kwa hilo.
Hata hivyo, Gadna alisema hajajua Lady Jay Dee anaitiwa nini na kwa sababu ya nani zaidi amemwelezea na amesema watatekeleza wito huo wa kufuka Jumatatu Mahakamani hapo.
Aidha, kupitia kwenye ukurasa wake wa Kijamii wa facebook,  Lady Jay Dee aliandika: “Ratiba ya Usiku wa leo,  ni Machozi Band, kama kawaida, ila ratiba ya Jumatatu natakiwa Mahakama ya Kinondoni..Taarifa zaidi zitafuata nikijua kinachoendelea...” aliandika Jide  kwenye ukurasa huo ambao mpaka hatua ya mwindishi anatembelea ‘post’ hiyo ilikuwa na maoni mengi ambayo watu mbalimbali walipata kuchangia.
Maoni hayo yanayokaribia zaidi ya 558 na, ‘Like’ zaidi ya 756 na ‘Share’ zaidi ya 20,  ambapo wengi wao wameweza kumuhusisha moja kwa moja na Mkurugenzi wa Clouds Fm, Ruge Mutahaba kuwa ndie aliyefanya hivyo.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali na moja ya gazeti hivi karibuni ilimnukuu Ruge kuwa amejiandaa kuchukua hatua  ikiwemo ya kisheria dhidi ya Lady Jay Dee baada ya kumsema kupitia kwenye mitandao ya kijamii.
**
Aidha, katika kuelekea shoo yake ya Miaka 13 ya Lady JayDee, amemtangaza rasmi msanii machachali wa bongofleva, Juma Nature.
Jide alisema Nature ameongezeka katika list ya wasanii watakaokuwepo kushiriki miaka 13  ambapo ataungana na wasanii wengine wengi siku hiyo  ambapo tayari tiketi zimeanza kuuzwa. “Naomba mujitokeze kwa wingi na tiketi zinapatikana karibu sehemu zote ikiwemo Shear Illusions Mlimani City, City Sports Lounge Mjini Posta, BM Salon Kinondoni, American Nails n Hair Salon,  bila kusahau Nyumbani Lounge mahala patakapofanyika shoo hiyo

BENITEZ ,JUU ,JUU ,JUU ,ZAIDI KAUWA UGENINI HUKU AKIAMBULIA KADI NYEKUNDU

.
Benteke 
 GOAL- Aston Villa 1-0 Chelsea - Christian Benteke (14 mins)Umekuwa msimu mzuri kwa Raia huyu wa Belgian! Anaipatia Aston Villa goli la kuongoza hakuna cha kusahangaza . Christian Benteke anafunga goli akipitisha mpira chini nahodha JT na Mlinda Mlinda Mlango Czech  kazi kwa  Brad Guzan, Yacouba Sylla waliomchezesha  Benteke, na ameshinda Gary Cahill kabla hajaingiza mpira wavuni .

Aston Villa 1-0 Chelsea

Kijana wa kibelgiji na asisli ya kongo akishangilia goli .
Benteke


Aston Villa 1-1 Chelsea


 Frank Lampard
GOAL - Aston Villa 1-1 Chelsea - Frank Lampard (61 DK)
Woow  I  Chelsea ilichokozwa na sasa! Frank Lampard anafunga goli tena la  202nd kwa   Chelsea, akipokea pasi kutoka kwa  Hazard,akiuzungusha mpira kwa mguu wa kushoto mita 15  .
Ni jambo zuri kwa Chelsea sasa 
 
Frank Lampard
GOAL - Aston Villa 1-2 Chelsea - Frank Lampard (88 DK)
A huge moment!
Frank Lampard Anafunga goli la pili kuongeza bao lake la 203 kwa mtindo wa aina yake . waligongeana pasi nasi na  Eden Hazard na kumpa nafasi ya kufunga  Lampard ambaye anaoneka shujaa wa mchezo .

Nafasi Timu P            GD          Points
 1 Man Utd 36 42 85
 2 Man City 36 31 75
 3 Chelsea 37 35 72
 4 Arsenal 36 31 67
 Stiliyan Petrov
Naama anavaa jezi namba kumi na Tisa pale Aston Villa katika uwanja wa Villa Park ilipotimu dakika ya 19th  - Jezi hiyo ilikuwa inavaliwa na Nahodha Stiliyan Petrov. na alikuwepo kiwanjani kukweli lilikuwa tukio la aina yake  .
klabu yake zamani ya Celtic ilifanya kama hivyo katika mechi yao dhidi ya  St Johnstone leo
 
 Petrov
 

YANGA WAANZA MAZOEZI LEO PEMBA KATIKA KUJIWINDA NA MECHI DHIDI YA SIMBA MEI 18

Wachezaji wa Young Africans Sports Club wakiwa mazoezini leo asubuhi katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba


Kikosi cha mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013 timu ya Young Africans Sports Club leo asubuhi kimeanza mazoezi katika uwanja wa Gombani mjini Pemba kujiandaa na mchezo wake wa mwisho dhidi ya timu ya Simba SC, mchezo utakaofayika mei 18 katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Yanga ambayo tayari ilishatwaa Ubingwa wa VPL kabla hata ya Ligi kumalizika imewasili salama kisiwani Pemba ambapo leo asubuhi kocha mkuu Ernie Brandts ameongoza mazoezi ya kikosi hicho kinachojiwinda kupata pointi 3 dhidi ya Simba Sc.
Ikiwa imebakia takribani wiki moja kabla ya mchezo wenyewe kufanyika, uongozi wa klabu ya Yanga kwa kushirikiana na benchi la ufundi uliamua kubadilisha mazingira ya kambi kutoka makao makuu ya klabu mpaka kisiwani Pemba kuhakikisha wachezaji wanapata mafunzo katika hali iliyo tulivu zaidi.
Akiongea mara baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, kocha Brandts amesema amefurahishwa kwa mapokezi ya wakazi wa kisiwa cha Pemba, kwani licha ya kuja kuweka kambi ya kujianda na pia wamepata fursa ya kubadilisha mazingira na kujifua vizuri katika hali iliyo tulivu.
Kuhusiana na hali ya kikosi Brandts alisema kikosi chake kipo fit kiaklil, kifikra na morali ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo hali inayoendelea kumpa uhakika zaidi wa kuondoka na pointi 3 katika mchezo huo wa mei 18.
Aidha Brandts akliongeza kuwa wachezaji wangu wote wapo salama, hakuna mgonjwa wala mchezaji majeruhi hivyo kuja kuweka kambi kisiwani Pemba kumeniongezea fursa ya kukaa na wachezaji wangu wote kwa pamoja, kuwapa mbinu mbalimbali kwa pamoja na kupanga jinsi ya kuibuka na ushindi dhidi ya Simba SC.
Uogozi wa klabu ya Yanga unawaomba wapenzi, wanachama na washabiki wake wote kwa pamoja kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa mei 18 dhidi ya Simba Sc kwani licha ya kucheza na watani wa jadi pia itakua ni siku ambayo Yanga itakabidhiwa rasmi kombe la Ubingwa wa VPL 2012/2013.

HIKI NDICHO KIKOSI BORA ZAIDI CHA FERGUSON KUPATA KUTOKEA MAISHANI MWAKE XI

Kwa hakika hivi vimekuwa vikosi Bora zaidi  Hasa unapuzungumzia  XI Bora za Sir Alex Ferguson ambavyo amewahi kuvipanga kiwanjani .
Huwezi kupingana nae wala kuongeza jambo katika hili  ,Ukianza Na mlinda mlango mahili kiwanjani ambaye alikuwa mkali kiwanjani  Peter Schmeichel. ambapo mbele yake akiwa na ukuta imara ambao ulikuwa ukiongozwa na , Gary Pallister na  Steve Bruce ambao walitengeneza maelewano mazuri sana kiwanjani , ukuta ambao mwandishi wa makala hii anasema haujawahi kutokea .anasema mbali ya hapo sehemu ya kiungo ilikuwa hatari zaidi kwani kulikuwa na kijana hatari Paul Ince ambaye tulikuwa nyuma yake alikuwa anajua nini cha kufanya kiwanjani .
Mark Hughes alikuwa hatari zaidi kwani alikuwa na miguu yenye nguvu zaidi na alikuwa na uwezo wa kuchukua mipira huku pembeni akiwa na kijana mfaransa Eric Cantona’s ambae alikuwa na uwezo wa hali ya juu katika kupiga chenga na kumiliki mpira kikosi kilimaliza ukata wa miaka 26 kutoka bila kikombe
1995-1999: VIKOMBE VITATU 
Miaka michache iliyofuata timu ilibadilika na Ferg alitengeneza vijana wenye vipaji vya aina yake kama  Gary Neville, David Beckham, Paul Scholes na  Nicky Butt ambao waliungana na  Giggs . hapo ulikuwa lazima uchanganyikiwe kwani katikati mwa kikosi hicho palikuwa na
  Roy Keane na  Scholes ilibidi ukubali upekee wa sehemu ya kiungo wa wachezaji hawa  kwani walitengeneza timu ya aina yake lakini timu hiyo ilikuwa na wachezaji wawili mapacha hatari zadi ambao unaweza kufikili kuwa walikuwa wamezaliwa siku moja au pamoja lakini sio kweli kwani mmoja ni raia wa uingereza na mwingine anatoka visiwa vya kule caribean tunawazungumzia   , Andy Cole na  Dwight Yorke ambao walitengeneza seshemu kali zaidi ya ushambuliaji  .
Teddy Sheringham na  Ole Gunnar Solskjaer na kijana kutoka  Tobago   walidhihirisha , bila shaka , siku ambayo waliushangaza ulimwengu baada ya kufunga mabao mawili na kuimaliza  Bayern Munich na kushinda ligi ya mabingwa ulaya mwaka  1999 .
Kwa wakati huo  Schmeichel alichaguliwa na kujulikana kuwa ndiye mlinda mlango bora zaidi ulimwenguni .hakika hata nje ya kiwanja kwa maana ya benchi la akiba kulikuwa na vijana kama  Jaap Stam,kijana hatari zaidi ambaye alikuwa tayari . hakuwa peke yake  Ronny Johnsen, Henning Berg  au Wes Brown wakiwa pamoja , Mholanzi huyo , hakika ulikuwa huwezi kushinda makombe kama haukuwa na kikosi kama hicho .
2006-09 Mwaka wa mafanikio tena ulaya 
Baada ya miaka miinne bila ubingwa wa Ligi ya uingereza alitengeneza kikosi kingine ambacho kilikuwa na wachezaji bora zaidi lakini hawakulingana sana na wale wa mwanzo na alikuja na mfumo wa  4-4-2.
,alinunua wachezaji kadhaa ambao waliweza kukabiliana na mfumo wake pamoja na Cristiano Ronaldo, aliweza kushabihiana na  Wayne Rooney na aliongezeka kijana mwingine mwenye nguvu  Carlos Tévez ambao walifanya kazi kubwa zaidi kiwanjani .kikosi hiki kiliweza kutwa ubingwa wa ulaya katika fainali iliyochezwa kule
 Moscow dhidi ya Chelsea. Baada ya Schmeichel,walipita walinda milango wengi lakini  Edwin van der Sar alipokuja mholanzi huyu ailipata raha golini kwani alikuwa akisaidiwa na ukuta bora  ambao ulikuwa ukiongozwa na  Rio Ferdinand na  Nemanja Vidic , Ferguson aliendelea kujikusanyia nishani katika soka . mzee alikuwa akijivunia kundi la watu shupavu . Giggs, Nani na Ji-Sung Park ambaye alisaidiwa na  Dimitar Berbatov ambaye alisajiriwa kuongeza radha tofauti katika nafasi ya ushambuliaji
2012-13 Kizazi kipya 
Ferguson anakielezea kikosi chake cha sasa kuwa kina uwezo wakufanya mambo makubwa zaidi siku za usoni kikiwa na wachezaji wadogo zaidi kama akina  David De Gea, Phil Jones, Chris Smalling, Rafael, Danny Welbeck na  Tom Cleverley – wakiwa chini ya miaka  24 wakiwa na mengi ya kujifunza .
Lakini anaweza kuwa chagua. Jones na Smalling, Bila shaka  ,Wanauwezo wa kupigana na kuuonyesha ulimwengu kuwa watakuwa mabeki bora katika safu ya ulinzi ya katika miaka ijayo .
Kutoka na Umri wa  Ferdinand’ na majeruhi yasiyokwisha na bila kusahau matatizo kama hayo yanamkabili pia Vidic, muda wao wa kuwepo klabuni hapo unawaka kwa taa ya nyekundu . Kwa sasa, Jones anastahili  nafasi katika kikosi manchester united bado ina hazina kubwa sana ya kujivunia hasa katika soka kwani huwezi kuacha kusema kutakuwaje msimu ujao pale wachezaji kama Zaha, Van persie ,Shinji kagawa na wengine ambao unawafahamu watakapo ungana na David Moyes je kitashuka au kitapanda 
.
Na mwisho ...Hiki ndio kikosi bora kwetu  
 Fergie XI

SUPER AJA NA DVD ZA MASUMBWI KWA AJIRI YA MAFUNZO KWA MABONDIA

 
Kocha  wa mchezo wa ngumi nchini,Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia  wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali

CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa hali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live maana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata dvd hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
 
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila ,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe. 
 
 mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers