HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 March 2014

CITY CHALI NOU CAMP ,PSG YAMALIZIA KIPORO ULAYA

Lionel Messi

Goli la Dani Alves' limeipatia ushindi  Barcelona Dhidi ya  Manchester City ambalo linawapeleka katika hatua ya robo fainali .

Wakiwa wanataka kujikwamua kwa kufungwa bao mbili sifuri mechi ya mwanzo , City's walipata nafasi Bora zaidi katika kipindi cha kwanza ambapo  Samir Nasri alipiga shuti lakini liliokolewa na mlinda mlango Victor Valdes.
Lionel Messi alimalizia pass iliyopigwa na  Cesc Fabregas na kufungwa la la kwanza kabla ya  Pablo Zabaleta kuonyeshwa kadi Nyekundu ambapo kabla alikuwa na kadi ya manjano .
Vincent Kompany aliifungia timu baada ya mpira wa kuparazwa kichwa kutoka kwa  Edin Dzeko's lakini Alves alifunga goli la ushindi akiunganisha mpira wa krosi kutoka kwa  Andres Iniesta's . 
Marquinhos 
Paris St-Germain imefuzu katika hatua ya mtoano kwa msimu wa pili baada ya kuifunga   Bayer Leverkusen ambao walikuwa wakicheza kumi kiwanjani.
Wakiwa wako nyuma kwa mabaoa manne kwa bila mechi ya kwanza , Leverkusen walipata goli kutoka kwa Sidney Sam.

Kichwa kilipigwa na Marquinhos's kilikwenda moja kwa moja wavuni na kuisawazishia  PSG huku Leverkusen's Simon Rolfes akikosa penati .
Ezequiel Lavezzi aliwapatia wenyeji goli la uongozi akipiga shuti katika umbali wa mita 14 , Kabla  Emre Can hajapigwa kadi ya pili ya manjano kwa kujirusha , huku PSG ikisonga mbele kwa jumla ya magoli sita kwa moja6-1 .
Mabingwa hao watetezi wa ligi ya ufaransa walifungwa msimu uliopita na  Barcelona katika hatua ya Robo fainali Lakini, Haijafungwa katika uwaja wake wa Nyumbani katika mashindano ya ulaya Tangu 2006, wanaweza kuamini kuwa watashinda michuano ya ulaya kwa ya kwanza tangu timu hiyo ianzishwe .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers