HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

10 March 2014

TFF YADAIWA MILION 15 NA SERIKALI




SERIKALI IMETOA TAMKO KUHUSU UHARIBIFU WA VITI ULIOTOKEA KATIKA MCHEZO KATI YA TIMU YA YANGA YA TANZANIA NA AL-AHLY YA MISRI  ULIOFANYIKA KWENYE UWANJA WA TAIFA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 01 MACHI, 2014. 
 WAKATI WA MCHEZO HUO, KULITOKEA VURUGU KUBWA ZILIZOFANYWA NA WATAZAMAJI AMBAPO BAADHI YAO WALING’OA VITI NA KUSABABISHA UHARIBIFU MKUBWA.  KATIKA VURUGU HIZO, VITI 10 VILING’OLEWA NA KUTUPWA NA ZAIDI YA VITI 40 VILIHARIBIWA.

SERIKALI IMESIKITISHWA SANA NA TUKIO HILI NA HASA KWA KUZINGATIA JITIHADA KUBWA ZILIZOFANYWA KUHAKIKISHA KUWA NCHI YETU INAKUWA NA VIWANJA VIZURI NA VYA KISASA NA HIVYO KUTOA FURSA KWA WANANCHI WAKE KUCHEZA NA KUPATA BURUDANI KATIKA VIWANJA BORA VYA KISASA NA SALAMA.

WIZARA IMEIELEKEZA TFF KUCHUKUA HATUA KALI KWA WOTE WATAKAOBAINIKA KUHUSIKA NA VURUGU HIZO NA KWA KUZINGATIA TARATIBU ZOTE.

TFF IMEPEWA MAELEKEZO HAYO KUTOKANA NA UKWELI WAO NDIO WASIMAMIZI WA MCHEZO HUO NA NDIO WALIOOMBA KUTUMIA UWANJA.

KIMSINGI, ENDAPO MATUKIO HAYO HAYATAKOMESHWA SERIKALI ITALAZIMIKA KUCHUKUA HATUA KALI ZAIDI.  IFAHAMIKE KUWA UWANJA NI MALI YA WATANZANIA WOTE NA HIVYO NI WAJIBU WA KILA MMOJA WETU KUULINDA NA KUUTUNZA KWA MANUFAA YA MAENDELEO YA MICHEZO NCHINI.

KWA JUMLA, WIZARA HAITAVUMULIA UHARIBIFU HUO KUENDELEA.  TUSINGEPENDA KUFIKIA HATUA YA KURUHUSU UWANJA KUTUMIKA BILA WATAZAMAJI AU KUZUIA BAADHI YA MICHEZO KUFANYIKA HAPO KAMA INAVYOTOKEA KATIKA NCHI NYINGINE.  NI VEMA TUKAENDELEZA USTAARABU WETU NA KUWA WAUNGWANA KILA TUNAPOKUWA UWANJANI KUZISHANGILIA TIMU ZETU.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers