HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

18 April 2014

JMOSI YA NGUMI NA KANDANDA DAR (RADIO CONFERENCE )

PLAY
 
Baada ya kuharishwa mpambano wa ngumi usio na ubingwa kati ya francis Cheka na Bondia kutoka Jamhuri ya kiislamu ya watu wa Iran Gavad Zohrehvand leo wamepima tena uzito katika ukumbi wa hotel ya Atriums majira ya saa tano asubuhi tayari kwa pambano lao litakalofanyika mwishoni wa Mwa wiki hii katika ukumbi wa PTA saba saba jijini Dar es salaam .
Awali pambano hilo ilibidi lifanyike jumamosi iliyopita lakini ilishindikana baada ya kuharishwa kutokana na mvua kali iliyokuwa ikinyesha katika jiji la Dar es salaam na kusababisha Madhara makubwa kwa wananchi na kuathiri pambano hilo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na watanzania .

Aidha pambano hilo lilitarajiwa kutanguliwa  na mpambano wa mwingine kati ya Bondia kutoka Tanzania  Fransic Miyeyusho 'Chichi' Mawe na  Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand  mapambano hayo yalitarajiwa kutanguliwa na mapambano ya masumbwi kati ya mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atakae pambana na Mustafa Doto mpambano wa Raundi sita pia kutakuwa na mapambano mengi ya utangulizi yatakayosindikiza mchezo huo.
Zoezi la kupima uzito limefanyika leo katika ukumbi wa Atriums uliopo afrika sana sinza jiji Dar es salaam mpambano hutachezwa siku ya jumamosi saa kumi na mbili jioni ilikupisha pambano la simba na yanga 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers