HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

8 August 2014

SIMBA NA COAST UNON KATIKA DUNIA YA UJIMA !

 
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema kuwa umekiri kupokea barua kutoka kwa kitengo cha
Wanasheria (Maleta& Ndumbaro Advocate ya Dar) ikisema kuwa timu hiyo imeshindwa kumlipa Abdi Banda mshahara wa miezi mitatu mfululizo kwa kusema imevunja mkataba.

Akizungumza jana,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi  amekanusha kwa kusema kuwa habari zilizoenezwa kuwa walishindwa kumlipa mshahara mchezaji huyo sio za kweli bali kilichotokea ni kwamba banda alifundishwa na watu wajinga kwamba asichukue mishahara yake ya miezi
mitatu ili kukipa hadhi kipengele hicho cha sheria kilichopo kwenye mkataba wake,

  “Akinukuu kipengele cha ibara ya 3(3.2)(1) cha mkataba wa Banda kinachosema kuwa ikiwa klabu imeshindwa kumlipa mchezaji mishahara yake ya miezi mitatu mfululizo basi mkataba wa mchezaji huyo na klabu umevunjika “Alisema El Siagi.

Alisema lakini alichokifanya mchezaji Banda ni kukwepa kuchukua mishahara yake makusudi ili ionekane kwamba hakulipwa miezi mitatu .

El Siagi alisema alichokifanya ni mambo mawili, jambo la kwanza ni kudanganya wanamichezo hapa nchini na klabu yake ya Coastal Union ili aipatie fedha Klabu ya Simba ambao huo ni Wizi wa kutumia hila.

Alisema la pili ni kitendo cha kusaini mkataba Simba wakati akijua ana mkataba na Coastal Union ambao unatarajiwa kuishia Juni 2016.

Katibu huyo alisema ni makosa makubwa mchezaji huyo kusaini mikataba miwili tofauti katika kipindi cha msimu mmoja kwa sababu atakuwa amevunja taratibu za mikataba kutokana na kuwa mchezaji hawezi kuwa na mikataba miwili kwa wakati mmoja.

Aidha alisema kutokana na mchezaji huyo kudanganya na kukiuka utaratibu wa mkataba, Uongozi wa  Coastal Union umejipanga kumchukulia hatua kali mchezaji huyo ikiwemo hatua za kinidhamu.

Katibu huyo alisema anashangazwa kuona kuwa klabu ya Simba yenye viongozi wazoefu kwenye masuala ya mpira wanafanya makosa kama hayo kwa kutokufuata taratibu za kiusajili.

   “Kanuni za shirikisho la soka Dunia (FIFA) na Shirikisho la soka nchini (TFF) zinasema mchezaji hawezi kuzungumza na timu yoyote wakati akiwa ndani ya mkataba mpaka labda awe amebakiza miezi sita kwenye mkataba wake ndio anaruhusiwa kuzungumza na uongozi wa klabu nyengine.

Aliongeza kuwa iwapo mchezaji akiwa amebakiza mwaka mmoja basi klabu na klabu ndio zinaruhusiwa kuongea na sio mchezaji hivyo Banda bado ana miaka miwili Coastal Union ambayo imebaki hivyo Simba walichotakiwa kufanya ni kuzungumza na uongozi wa Coastal union ili
kumnunua mkataba wake badala ya kurubuniwa na kauli hafifu za kiudanyanyifu.

Katibu huyo alisema kwa kufanya hivyo Coastal Union kupitia wanasheria wake ,Divine Chambers Advocates & Hamidu Mbwezeleni wanajipanga kuwaandikia barua shirikisho la soka nchini (TFF) pamoja na Simba ili
kudai fidia ya Ukweukwaji wa taratibu hizo.

Alieleza kuwa tayari Coastal Union wamemtumia mwanasheria wa Banda majibu ya barua yake kupitia mwanasheria Divine Chambers Advocates ya Mjini Tanga

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers