HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

7 September 2014

MALINZI NANI KAKUSHAURI KUHUSU AFCON ?


 

Naam  Tangu aingie madarakani kuchukua Kjiti kilichoachwa na Leodgar Chila Tenga  Ndoto yake kubwa imekuwa ni kuiona Tanzania ikishiriki michuano ya Afrika yaani AFCON . na sasa inavyoona nekana ni kwa njia yoyote ile iwe ya kufuzu au kuandaa mashindano hayo lakini sio tatizo wala sio shida kwa Tanzania Kundaa mashindano hayo Tatizo ni muda.

Mashindano ya AFCON Mwaka 2017 ilibidi yaaandaliwe na Libya ambayo tangu kung'olewa kwa Kiongozi wa Nchi hiyo Marehemu kanali Muamar Gadafi, Amkani si shwari tena  kwa Nchi hiyo wakaamua Kujitoa sasa inatafutwa nchi Mbadara wa Kuandaa fainali hizo moja ya Nchi zilizoomba ni kenya Tanzania pamoja na Uganda japo kenya na Uganda zimeonyesha nia ya Kuandaa kwa mashirikiano huku Tanzaia ikiwa na wazo kama hilo kwa kushiriakiana na kenya .

Naam ngoja tuitazame Tanzania ambayo inataka kuandaa Mashindano hayo ambapo kwa mujibu wa Shirikisho wanasema serikali itaunga mkono jambo hilo .

Changamoto ninazoziona kwanza kabisa kwasasa viwanja ambavyo tunavyo vya maana vya kuchezea mechi za kimataifa ni viwili ambacho kimoja kina mashaka, Uwanja mpya wa Taifa na ccm kirumba mwanza .

Ukitazama uwanja wa Taifa baadhi ya Vitu vimeshahalibiki vikiwemo viti ,vyoo,na vitu vingi ambavyo kama watavifanyia uchunguzi inawezekana kuna mambo mengi ambayo yamekwisha halibika na huo ni uwanja mpya wa taifa sijui uwanja kama ccm kirumba ambao ni wa miaka mingi .

tukishirikiana kuandaa na kenya ina maana tutakuwa na timu nane Tanzania. ambapo tutakuwa  na viwanja nane vizuri vya mazoezi na itagemeana katika makundi kuna timu za aina gani maana kuna timu nyingine zinaweza kugomea hata viwanja .

Hotel kwa timu hizo nane sidhani kama tunazo kama kwenda kuweka timu kwenye Hotel za nyota mbili ambazo hatakiwi kabisa
Mwakani Tanzania itakuwa Inaingia kwenye uchaguzi mkuu Tatizo jingine  ambalo kama tunavyojua itakuwa imebakia miaka miwili kuandaa michuano hiyo na kama kawaida ya Nchi yetu uchaguzi wa Nchi hii hutumika pesa nyingi sana na huwa hatujui zinatoka wapi maana kama zingetumika kimaendeleo tungekuwa mbali sana.

Na Huwezi jua nini kitatokea kwani Mchakato wa kutafuta katiba mpya Ungali unaendelea 
hii inamaana kuwa Tanzania kuna sinema tatu zinazokuja ambazo bado haijajulikana nani atakuwa mshindi wa sinema hizo.

Ukirejea katika mfumo wa Ligi ya Tanzania Bado kuna changamoto kadhaa ikiwemo tiketi za kieletronick,ununuaji wa tikiti kwa mitandao,mindombinu ya kiusafiri hivi ni kweli Rais Malinzi anatakakuandaa tu kwa utani tuu au kwa umakini?  Binafsi ninamshauri angejiandaa hata kwa mwaka 2021 kidogo tungemwelewa lakini kwa sasa sidhani kama kashauriwa vizuri.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers