HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

19 November 2014

AZAMFC YAMTAKA KIEMBA KWA MKOPO(SIKIZA SAUTI)
Mabingwa wa soka Tanzania bara Azam FC wametangaza dhamira yao ya kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Simba Amri Ramadhan Kiemba ambae kwa sasa bado anasubiri hatama yake kutoka kwa viongozi wa klabu hiyo ya Msimbazi kufutia tuhuma za kucheza chini ya kiwango katika michezo mitano ya kwanza ya ligi kuu.

Mwenyekiti wa klabu ya Azam FC, Sheikh Said Muhammad Abeid amesema tayari wameshawasilisha ofay a kutaka kumsajili Kiemba baada ya kocha wao kutoka nchini Cameroon Joseph Omog kumpendekeza miongoni mwa wachezajia mbao angependa wasajiliwe katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili..
Hata hivyo mwenyekiti huo wa Azam FC amesema dhumuni lao kwa kiemba ni kumsajili kwa mkataba wa mkopo akitokea Simba na si kumsajili moja kwa moja kama walivyoanza kufanya kwa beki kutoka nchini Ivory Coast Serge Wawa akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Sudan El Merekh.

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa klabu ya Azam FC, Sheikh Said Muhammad Abeid amekiri kusikitishwa na mwenendo mbovu wa klabu ya Mbeya City ambayo kwa msimu huu ulioshuhudia michezo saba mpaka sasa imeshindwa kufanya makubwa kama ilivyokua msimu uliopita ambapo walicheza ligi kwa mara yao ya kwanza.


No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers