12 November 2014

MICHUANO YA MBIO NDEFU INAUA MBIO FUPI (SIKIZA RADIO)




Shirikisho la mchezo wa riadha nchini RT linaandaa mkakati utakaowabana waandaaji michuano ya mbio ndefu ambayo hufanyika kila mwaka, ili kuwawezesha wanariadha wanaokimbia mbio fupi kunufaika na michuano hiyo.

Katibu mkuu wa RT Suleyman Nyambui amesema kwa sasa wamebaini, michuano ya mbio ndefu ambayo hufanyika zaidi ya mara tatu kila mwaka, imekua inashindwa kuwaendeleza vijana wenye malengo la kushindana katika mbio fupi kutokana na mchezo huo kutoshirikishwa kikamilifu.
CHEZA HAPA 
 

Hata hivyo Nyambui amesema wanaamini kuutambulisha mpango huo wa kushirikisha mbio fupi kupirtia michuano yam bio ndefu, kuanzia mwaka 2015 bado haujachelewa kutokana na vijana wengi kuwa katika mikakati ya kukuzwa kupitia michuano mbali mbali ya shule za msingi na sekondari.

No comments:

Post a Comment