23 May 2009
HAYA NDIO MAFUNZO YA KUOGELEA KWA WATOTO
MASHINDANO YA WAZI YA KUOGEALEA KATIKA BWAWA LA TANNGANYIKA
INTERNATIONA SCHOOL
Moja kati ya vitu vya msingi katika michezo ni kuandaa timu hasa katika umri mdogo kama unakumbuka vizuri katika michuana ya Olympic iliyo fanyika huko Beijing china Muogeleaji mahiri wa marekani Michael Phelps aliweza kuibuka kinara kutokana na umahiri wake wa kuogerea katika michezo hiyo ya Olympic lakini unaweza kuwa mwanzo mzuri kwa Tanzania ambapo kwa sasa kwani katika kila aina ya mchezo hii inaonekana kuna ni ya kuifanya michezo hiyo kuwa katika kiwango cha juuu kutokana maandalizi mazuri ndicho nilicho kiona katika bwawa shule ya Tanganyika international school iliyopo Upanga jijini dar es salaam wakati watoto wengi walipokuwa wakijifua katika mashindano ya wazi ya kuogelea ambapo walikuwa wakionyesha umahiri wa hari ya juu sana wakifuata sheria zote za mchezo huo.
Hawa ndio watakao kuwa mashuja wetu wa baadae tukiwatunza
watoto chini ya umri wa miaka kumi wakiaogelea katika mashindano ya wazi kutafuta vipaji vya kuogelea
Naam kwa mfumo huuu ni dhahiri kwamba tutafanikiwa na tunaweza kufika mbali kwani hata hao wakina Michael phelps wa marekani walianza mambo haya wakiwa katika umri mdogo zaidi na ndiyo maana wakaweza kutwaa medali nyingi katika Michezo ya Olympic kule China nina imani kabisa kwamba kama juhudi zitafanyika basi Tanzania tuatatoa wanamichezo wengi zaidi miaka ijayo kwani kuwekeza katika vijana wenye umri mdogo ndio mwanzo mzuri wa kufanikiwa michezoni.
kama unaweza kuona moja kati vijana wakiwa kazini wakkata maji kwa umahiri mkubwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
lisungu_chisara@yahoo.com
TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA
No comments:
Post a Comment