7 May 2009
wanajeshi colombia matatani
Wanajeshi 24 akiwemo kanali mmoja na kapteni mmoja wametiwa nguvuni kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watu wasio na hatia kwa kisingizio kuwa wao ni waasi nchini Colombia.
Inakisiwa kuwa maelfu ya watu wameuawa katika opereshini hiyo haramu iliokuwa ikiendeshwa na wanajeshi hao.
Ofisi ya mkuu wa sheria nchini humo inafanya uchunguzi wa kesi mia tisa ambapo watu elfu moja mia tano waliuawa kinyama na vikosi vya usalama.
Mwezi october mwaka jana, wanajeshi 27 wakiwemo jenerali watatu na makanali kumi na moja walifutwa kazi kufuatia madai kuwa walihusika na mauaji ya watu wasio na hatia au walizembea kazini na kuwaachia vikosi vyao kutekeleza mauaji hayo ya kinyama.
Waziri wa ulinzi, Juan Manuel Santos, ambaye pia anatarajia kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka ujao, kipindi hicho alisema mauaji kama hayo na ukiukaji wa haki za binadamu hautotokea tena.
Lakini visa hivi ni ishara ya kuwa ahadi hiyo haijatimia.
Ingawa wengi wa wanajeshi waliokamatwa sasa walihusika na mauaji yaliofanyika mwaka wa 2004, kumekuwepo na kesi mbili za mauaji ya aina hiyo tangu Octoba mwaka jana.
Kashfa hii inamharibia sifa Rais Alvaro Uribe. Tayari serikali ya Uingereza imetangaza kuwa imeacha kutoa misaada ya kijeshi kwa nchi hiyo.
Marekani nayo inatizama upya ahadi yake ya misaada inayogharimu dola milioni mia sita, kiasi kikubwa kikiwa kimelenga kusaidia jeshi la Colombia.(BBCSWAHILI)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
lisungu_chisara@yahoo.com
TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA
No comments:
Post a Comment