18 June 2009
Upinzani nchini Iran leo imeapnaga kufanya Maandamano kuomboleza vifo vya wenzao waliyouwawa katika ghasia za kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais.
Maandamano hayo yametajwa kuwa na lengo la kuishinikiza mamlaka ya Kiislam ya Iran kutoyatambua matokeo hayo.
Tathimini inaonesha kuwa vurugu za sasa za kuwakamata wapinzani na baadhi ya wanaharakati na kuvipiga marufuku baadhi ya vyombo vya habari hazijawahi kutokea tangu mapinduzi ya nchi hiyo mwaka 1979.
Pamoja na hali hiyo Mgombea Urais aliyeshindwa Hussen Mousavi ametoa wito kwa wafuasi wake kuingia mtaani tena kufanya maandamano mengine.
Maandamano ya sasa pamoja na kupinga matokeo Mousavi amewataka wafuasi hao kuvaa mavazi meusi ikiwa ishara ya kuomboleza wenzao waliyopoteza maisha.
Awali Mamia ya Waandamanaji walijitokeza na kufanya maandamano ya kimya jana wakiwa wamefunga vitambaa vya kijani mkononi na kufunga rumundi ya rangi hiyo hiyo kichwani ambayo ni rangi ya kampeni ya Mousavi.
Aidha Waandamanaji hao pia walibeba mabango yanayomtuhumu Rais Mteule wa Iran Mahmoud Ahmadinejad kwa kuiba kura katika uchaguzi wa ijumaa iliyopita.
Televisheni ya Taifa ilionesha kidogo maandamano hayo ambayo yalifanyika pamoja na serikali kupiga marufuku mkusanyiko wa namna hiyo.
Watu saba wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa katika vurugu zilizotokea baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi.
Taarifa zinadai kuwa pamoja na mjini mkuu wa Tehran Waandamanaji waliyokuwa wanapinga matokeo hayo walitapakaa katika maeneo tofauti pia.
Kiongozi wa Kidini nchini Iran Ayatollah Alli Khameini amesema atatilia maanani malalamiko hayo kwa kurejea tena zoezi la kuhesabu kura.
Lakini Mousavi ameendelea kusisitiza kutaka kurejewa tena kwa zoezi la upigaji kura akidai kulifanyika udanganyifu mkubwa.
Mataifa mbalimbali Duniani kote yameonesha kusikitishwa na hali ilivyo nchini humo na hasa hali ya kukamatwa kwa watu na kuwekwa vizuizini.
Katika tukio la hivi karibuni Viongozi waasisi wa mapinduzi ya nchi hiyo waliowahi kushikia nyadhifa za juu serikalini Ebrahimu Yazdi na Mohammed Tavasoli wamekamatwa na kuwekwa kizuizini.
Mousavi mwenyewe na rais wa zamani wa Iran Mohammad Khatami ambao wote kwa pamoja walifanikisha kampeni iliyomuingiza madaraka Ahmadinejad mwaka 2005 wameandika barua ya pamoja kuitaka serikali ya Iran kuwachia huru viongozi hao wakongwe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
lisungu_chisara@yahoo.com
TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA
No comments:
Post a Comment