HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

28 October 2009

MAANDALIZI YA SIMBA SC NA YANGA SC

Katibu Mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela (mwenye shati la drafti) akizungumza na wanahabari jana akitangaza viingilio vya mechi ya Simba SC na Yanga FC Jumamosi katika uwanja mpya wa Taifa. Katibu Mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela akiongea na wanahabari leo kutangaza viingilio vya mechi ya Simba SC na Yanga FC Jumamosi katika wanja jipya la Neshno.Amesema viti vya kule Urusi (mduara wa kijani na buluu, juu kabisa) ni 5,000/- (kijani) na 7,000/- (buluu) wakati viti rangi ya chungwa nyuma ya magoli ni sh. 10,000/- na viti vya rangi ya chungwa kuangaliana na stendi ya VIP ni sh. 20,000/-Mwakalebela kasema viti vya VIP 'C' ni sh 30,000/- ambapo VIP 'B'ni sh 50,000/- na VIP 'A' ni sh 60,000/-Amesema tiketi hazitouzwa mlangoni siku hiyo ya mchezo na kwamba zitauzwa kwa siku tatu tu yaani kuanzia kesho Jumatano hadi Ijumaa. Ametaja vituo zitapopatikana tiketi hizo kuwa ni Benjamin Mkapa Secondary School, Big Bon za Kariakoo na Mbagala,Steers ya mtaa wa Ohio Street and Steers ya Makumbusho, Oil Com Ubungo na Oil Com VETA Chang’ombe.Vituo vingine ni uwanja wa Uhuru, Supco Petro Station (Mwembe Chai) Kobil Buguruni,, Ferry, njia panda Tabata, Police Post Tandika Mwisho,Mwembe Yanga Police Post na Mtoni Mtongani

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers