Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Rodger Tenga akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Movenpick leo wakati alipozungumzia ujio wa timu ya taifa ya Brazil itakayowasili nchini na kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Juni 7 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa.
Tenga amesema amesema anaishukuru TILOC na kamati iliyoundwa na rais inayoongozwa na Mwenyekiti Dr. Shukuru Kawambwa ambaye ni Waziri wa Miundombinu Shukuru kawambwa wamefanya kazi nzuri mpaka kufanikisha ujio wa timu hiyo bora duniani.
Brazil tayari imeshatua arfajiri ya leo nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya kombe la dunia ambapo itakuwa na michezo miwili ya kuijipima nguvu katika yake Zimbabwe na kisha na Tifa Stars ambapo itawasili na watu sitini kati ya hao 25 wakiwa ni wachezaji
HIKI NDICHOKIKOSI CHA BRAZIL KITAKOCHEZA NA STARS JUMATATU TAREHE SABA
Meneja uhusiano wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda akizungumza katika mkutano huo uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Movenpick.
kwa hisani ya fullshangwe.blogspot.com
No comments:
Post a Comment