Shirika la Kutetea haki za kibinadam la Amnesty International limeilaani vikali uamuzi wa serikali ya Libya wa kuwanyonga watu 18 wengi wao wakiwa raia wa mataifa ya kigeni.
Shirika hilo la Amnensty limenukuu habari kutoka kwa gazeti moja nchini Libya, linalomilikiwa na mwanawe kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muamar Gadaffi.
Ripoti hiyo iliripoti kuwa watu 18 wengi wao raia wa Misri na Nigeria, walinyongwa siku ya Jumapili, baada ya kupatikana na hatia ya kupanga mauaji.
Shirika hilo limesema limehuzunishwa na hukumu hiyo iliyotolewa nchini Libya baada ya kesi ambayo haitimiza masharti ya kimataifa kuhusu kusikilizwa kwa kesi kwa njia ya haki. http://www.bbcswahili.com/
No comments:
Post a Comment