TANZANIA imeanza vyema mashindano hayo kwa kushinda mechi yake ya kwanza kwa magoli 50 kwa 25 dhidi ya Lesotho.
Akifungua mashindano hayo naibu waziri wa michezo wa AFRIKA KUSINI GERT OOSHIZEN amesema kuwa mashindano hayo yanaimarisha mchezo huo na kuweka uhusiano mzuri baina ya nchi zinazoshiriki.
Mchezo mwingine ulikuwa kati ya ZIMBABWE na AFRIKA kusini ambapo timu hizo zimeonyeshana kazi kubwa kutokana na kila timu kujiandaa vilivyo ambapo AFRIKA KUSINI iliibuka mshindi kwa magoli 64 kwa 29.
Kwa upande wake kocha wa TANZANIA SIMONE MCKIWIS amesema mefurahia ushindi wa timu yake na kuahidi watanzania kuwa timu hiyo itaendeela kufanya vizuri katika michezo yake inayoendeela ambapo amewataka watanzania kuiunga mkono timu hiyo.
Hata hivyo mashindano hayo yamekosa msisimko mkubwa kutokana na mashabiki wachache kuhudhuria, tofauti na mashindano ya kimataifa yaliyofanyika nchini mwaka jana ambapo watu mbali mbali waliweza kuhudhuria.
Mashindano hayo yanashirikisha timu sita kutoka AFRIKA ambazo ni NAMIBIA, TANZANIA, BOTSWANA, LESOTHO, ZIMBABWE, na wenyeji AFRIKA KUSINI.
No comments:
Post a Comment