Timu ya Taifa chini ya miaka 23 imewasili salama Uganda jana saa 1.30 usiku
kwa ndege ya Air Uganda chini yz kiongozi wa msafara Hafidh Ally Tahir.
-U23 chini ya Kocha Jamhuri Kihwelo ''Julio'' imewasili na wachezaji 20;
Nahodha Shaaban Kado, Juma Abdul, David Luhende, Babu Ally, Shomari Kapombe,
Jabir Aziz, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, Kigi Makasi,
Gharib Mussa, Mbwana Bakari, Idrisa Abdulrahim, Innocent Wambura, Khamis Mcha,
Amour Suleiman, Himid Mao, Mrisho Ngasa na Salum Telela.
-Timu imefikia hoteli ya Sojovalo iliyoko Barabara ya Rubaga hapa Kampala. Leo
saa 1.30 asubuhi imefanya mazoezi kwenye uwanja wa klabu ya Express Red Eagles
ulioko Wankuluku.
-Jioni kuanzia saa 10 kamili timu itafanya mazoezi Uwanja wa Mandela (Namboole)
kwa kati ya dakika 45 na saa 1 kujiandaa kwa mechi ya kesho. Mechi ya kesho
dhidi ya Uganda 23 (The Kobs) inayofundishwa na kocha wa zamani wa Kagera
Sugar, George Ssemogerere itachezwa Uwanja wa Mandela kuanzia saa 10.30 jioni.
Baada ya mazoezi ya U23 ndiyo kutakuwa na mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre
Match Meeting) utakaofanyika kwenye ofisi za Shirikisho la Vyama vya Mpira wa
Miguu Uganda (FUFA).
-Uwanja huo utatumika kwa mara ya kwanza kesho, kwani kwa kipindi cha miezi
sita iliyopita haukutumika kutokana na kuwa kwenye ukarabati. Kobs walifanya
mazoezi yao ya leo asubuhi kwenye uwanja huo.
-Kocha Julio amesema wachezaji wake wote wako katika hali nzuri kwa ajili ya
mechi ya kesho. "Tuko vizuri, tumekuja kupambana. Tunajua Uganda ni timu nzuri,
lakini tumejipanga kwa ajili ya kupata ushindi ili kujiweka katika mazingira
mazuri kwa mechi ya marudiano itakayofanyika nyumbani,"amesema Julio.
-Amesema atataja kikosi kitakachoanza kesho asubuhi baada ya wachezaji kupata
kifungua kinywa.
-Mechi hiyo imekuwa ikizungumza katika baadhi ya viunga vya Kampala kutokana na
U23 kuitoa Cameroon kwenye michuano ya mchujo ya Olimpiki.
-Kikosi cha Kobs kina baadhi ya wachezaji wanaochezwa soka nje ya Uganda kama
Emmanuel Okwi (Tanzania) na Moses Oloya (Vietnam). Wengine ni Benjamin Ochan,
Ayoub Kisarita, Godfrey Walusimbi, Owen Kasule, Patrick Edema, Ivan Bukenya,
Sadam Mussa, Mike Mutyaba, Isaac Isinde na Diego Kiiza.
Best Regards,
Boniface Wambura
TFF Media Officer
0767310242
No comments:
Post a Comment