HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

2 September 2012

JAMHURI YAIZAMISHA FALCON NGAO YA JAMII


TIMU ya soka ya Jamhuri, imefanikiwa kubeba Ngao ya Jamii baada ya kuwafunga  mabingwa wa soka Zanzibar, Super Falcon kwa  cha mabao 3-1.
Katika mchezo  wa uzinduzi wa ligi kuu ya Zanzibar msimu wa 2012/13 inayodhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt, Super Falcon hawakuwa katika kiwango cha kuridhisha ambapo mlinda mlango  Suleiman Janabi, alifanya maskosa yalitosababisha kufungwa mabao mawili kati ya hayo
Pambano hilo lilifanyika katika uwanja wa Amaan majira  ya usiku na kupambwa na burudani mbalimbali za muziki, huku bendi ya mbwa kachoka nayo ikitumbuiza kiwanjani hapo .
Pamoja na kupoteza mchezo huo, Super Falcon ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuzifumania nyavu za Jamhuri kwa bao safi  dakika ya 15 lililopachikwa kimiani na Deo Cassian, aliyeunganisha vyema mpira wa krosi kutoka kwa Hemed Bakari.
  
 Mgeni Rasmi katika Mchezo wa ufunguzi wa  ligi kuu ya Zanzibar Grand Malt, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii (SMZ),Mh. Juma Haji Duni (kushoto) akimkabidhi Ngao  Nahodha wa Timu ya Jamhuri kutoka  Pemba,Ally Said Choma baada kuifunga  Super Falcon mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa jumamosi usiku kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar. Katikati ni Meneja Masoko wa Grand Malt, Fimbo Butallah

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers