Baada ya hapo jana kujitokeza mbele ya waandishi wa habari kwa wacheza filamu wa kike nchini Wema Sepetu na Aunt Ezekiel, wadau wa tasnia hiyo wamesema kitendo hicho ni cha kupongezwa na wasanii hao wanapaswa kusamehewa.
Hatua hiyo ya kuomba radhi kwa wasanii hao kilitokana na wao kupanda jukwaani wakiwa wamevalia vivazi vinavyo onyesha sehemu kubwa ya maungo yao
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Wema Sepetu alisema kuwa wanaomba msamaha kwa jamii nzima kwa kitendo kilichotokea kwani anaamini kuwa wameikosea jamii kwa ujumla ikiwa wao ni kioo cha jamii.

Msamahaa huo umekuja baada ya Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) kushinikiza na kukipigia kelele tabia hiyo kwa madai kuwa wanaishushia hadhi tasnia ya filamu nchini
Pamoja na hayo uongozi wa TAFF liliwaandikia barua za onyo wasanii hao kwa kitendo hicho walichokifanya huku Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lililaani tabia hiyo ya kudhalilisha sanaa ya filamu.
Wadau wanasema ni vema jamii ikawasamehe kwani wameonyesha ujasiri kwa kujitokeza hadharani na kukiri kufanya makosa na kwamba sasa tusahau yaliyopita na tuunge mkono sanaa zao.
No comments:
Post a Comment