HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

15 October 2012

TANZANIA (BFT) ALHAJ SHAABAN MWINTANGA AACHIWA HURU

Aliyekuwa  Rais wa shirikisho Ngumi za Ridhaa Tanzania (TBF) Alhaj Shaaban Mwintanga ambaye alikua  anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini kwa tuhuma za kuhusishwa na sakata usafirishaji   madawa ya kulevya aina ya Heroine yenye thamani ya mamilioni ya shilingi.
Kuachiwa huru kwa Mintanga kunatokana na mahakama kueleza kuwa, upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake.

Jaji Dk. Fauz Twaib, alitoa uamuzi huo jana, kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani mbele yake ili kuamua endapo mshitakiwa huyo ana kesi ya kujibu au la. Alikuwa akikabiliwa na mashitaka mawili ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa Jaji Twaib, upande wa mashitaka uliwasilisha mahakamani mashahidi wanne, ambao ni Christopher Mutarukwa, Nassoro Irenge, Emilia Poliano na Charles Ulaya.

Alisema ushahidi wa Ulaya umezua kuwepo kwa kujichanganya katika kesi ya upande wa mashitaka, ikiwemo uzito wa dawa za kulevya ambao kwenye hati ya kuonyesha thamani yake inaelezwa ni kilo 4.8 na kwenye kielelezo cha nukushi (fax) kutoka Mauritius inaonyesha ni kilo sita.

Jaji alisema ripoti kamili aliyopewa shahidi huyo hakuiwasilisha mahakamani kama kielelezo na hakuna shahidi yeyote aliyetoa ushahidi kuhusu idadi ya kilo za dawa hizo.

Alisema tangu awali aliyekuwa akitafutwa kuhusika na usafirishaji wa dawa hizo ni mtuhumiwa Mika na si Mintanga na kwamba, mtuhumiwa Msengwa ambaye anashikiliwa Mauritius kwenye maelezo yake alisema hamfahamu Mintanga.

Ulaya katika ushahidi wake alidai Msengwa alipatiwa dawa hizo na Mika katika hoteli iliyoko eneo la Manzese, Dar es Salaam na alikuwa akiwasiliana na mwanamke raia wa Kenya.

Jaji alisema upande wa mashitaka pia umeshindwa kuthibitisha mahali na tarehe ambayo washitakiwa walikula njama.

JANEJOHN.BLOGSPOT.COM/

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers