HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

7 November 2012

TAIFA STARS BOBAN WAACHWA KANAVARO HAJAKUMBUKWA.


KOCHA Mkuu wa timu ya taifa, ‘Taifa Stars’, Kim Poulsen, ametangaza kikosi cha wachezaji 22 watakaoingia kambini jijini Mwanza,kujiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji na mechi ya Kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya.

Katika kikosi hicho wachezaji wakongwe ni kipa Juma Kaseja,Ngassa,Aggrey Moris na Chuji, Nyoni, Shaaban Nditi,Amir Maftaha, Amri Kiemba, Yondani na Nasso Cholo

Akitangaza kikosi hicho mbele ya waandishi wa habari katika Hoteli ya La Kairo jijini Mwanza ,Poulsen alisema kuwa ametumia vigezo vitatu kwa ajili ya kupata wachezaji hao ambavyo ni vipaji, hamasa ya mchezji juu ya kuichezea timu yake ya taifa pamoja na nidhamu na kujituma uwanjani na kueleza kuwa katika kikosi hicho ametoa nafasi zaidi kwa vijana.

Alisema miezi sita iliyopita alichagua wachezaji makinda Frank Domayo na Simon Msuva na kitendo kilicho washangaza wananchi kutokana na uteuzi huo.

“Uteuzi wangu wa wachezaji vijana chipukizi, Frank Domayo na Simon Msuva, miezi sita iliyopita uliwashangaza wanachi, lakini vijana hao leo hii wanacheza mpira wa uhakika,”alisema Polsen
Aliwatetea vijana aliowateuwa katika kikosi hicho akisema anamini vijana watafanya vyema katika mechi zinazoikabili Stars na watakuwa hazina ya nchi hii siku zijazona kuomba wapewe ushirkiano kwa kuwapa nafasi ya kuitumikia timu ya Taifa.
Poulsen alisema amewaacha baadhi ya wachezaji kutokana na kuwa majeruhi,huku wengine viwango vyao vikiwa vimeshuka na wengine kufungiwa na timu zao kutokana na makosa mbalimbali.
Amesema mshambuliaji wa Yanga Said Bahanuzi ameachwa kwa sababu ya majeruhi, huku Ramadhani Chombo Redondo,akiachwa kwa kushuka kiwango chake pamoja na Haruna Moshi aliyefungiwa na klabu yaker ya Simba kwa utovu wa nidhamu.
Aliwataja wachezaji aliowateuwa kwa nafasi ya golikipa Juma Kaseja (Simba)na Deogratius Munish (AZam). Mabekini Nassor Masoud Cholo, Aggrey na Morris Erasto Nyoni (Azam) Kelvin Yondan (Yanga), Shomari Kapombe na Amir Mafutah (Simba) pamoja na Issa Rashid.
Viungo ni Ramadhan Singano, Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd 'chuji, Frank Domayo (Yanga), Shaaban Nditi (Mtibwa), Amir Kiemba Mwinyi Kazimoto pamoja na Mrisho Ngassa (Simba).
Poulsen amewaita washambuliaji John Boko(Azam), Simon Msuva (Yanga), Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu(TP Mazembe) pamoja na Edward Christopher (Simba).
Amesema kuwa timu hiyo inatarajia kuingia kambini Jumapili ya wiki hii na itakuwa ikifanyia mazoezi katika uwanja wa michezo waCCM Kirumba.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers