HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

15 November 2012

TENGA NAKUOMBA RADHI POPOTE ULIPO :SAAD KAWEMBA

Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la kandanda la Tff .
Saad Kawemba amemuomba radhi Rais wa shirikisho la kandanda la Tanzania Leodgar Chila Tenda ,
Mara baada ya moja ya watazamaji katika kipindi cha Tuongee Asubuhi Kinachorushwa na Star Tv ya Mwanza kumtuhumu waziwazi kuwa Rais wa shirikisho aache kupendelea na kutumbua pesa za shirikisho hilo.

Akijibu kwa hudhuni ya hari ya juu mkurugenzi wa mashindano ya tff ambaye yupo mwanza kikazi alijibu swali hilo kwa kusema kuwa Rais wa tff hausiki katika maamuzi ya aina yoyote ile yanayofanywa na baadhi ya kamati teule zinazosimamia mambo mbalimbali yahusuyo soka  katika shirikisho hilo.  Kawemba alisema kama Tenga angeamua kupendelea basi leo hii Pan Afrika isingeshuka daraja kwani ndiyo timu yake tena aliongeza kwa kusema kuwa timu hiyo imeshuka daraja wakati yeye akiwa Madarakani .

Kwa upande mwingine amesema hari ariyonayo Bwana Tenga kifedha ni kwa mambo yake mengine ambayo haiusiani kabisa na fedha za shirikisho hilo na sio mbadhilifu kama watu wanavyoweza kufikiri .
alimaliza kwa kusema kuwa Rais tenga hana sifa hizo kwani  ni moja kati ya viongozi waadilifu katika soka la tanzania na kusisitiza kuwa kila kamati imepewa majukumu yake na yeye huwa aingilii kamati ya aina yeyote ikiwemo ya usajiri.

Mtazamaji huyo ailipiga simu kutoka katika mkoa wa Mmoja hapa Tanzania ambapo alimtuhumu rais wa TFF kuwa amekuwa akipendelea moja ya klabu kubwa Tanzania na amekuwa akitumia pesa za shirikisho la soka kujinufaisha Binafsi  jambo lililomfanya kawemba kumuomba radhi rais Tenga  ambaye ilibidi aweke sawa kutokana kuwa alikuwa akiheshimu kipindi na mtazamaji aliyepiga simu.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers