Wachezaji wa timu ya taifa ya Zanzibar waliofungiwa mwaka mmoja na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kucheza soka mahala popote kutokana na madai ya utovu wa nidhamu, hawatatumikia adhabu hiyo hadi Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itakapokaa kujadili maamuzi hayo.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah amesema kuwa wameiandikia barua ZFA kuifahamisha kwamba wamepokea barua ya chama hicho cha soka inayowafahamisha kuhusu kufungiwa kwa nyota hao, lakini wameipeleka katika Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF kwa hatua zaidi, hivyo kwa sasa shirikisho litasubiri uamuzi wa kamati hiyo.
"Tumewaandikia barua ZFA, tumewafahamisha kwamba tuko pamoja na nidhamu ni lazima ilindwe, lakini kwa sasa wachezaji hawatatumikia adhabu hiyo hadi baada ya kikao cha kamati ya nidhamu," Osiah.
No comments:
Post a Comment