Jordan Ayew Ameachwa katika kikosi cha wachezaji 25 cha Ghana’s ambacho kitacheza mashindano ya mataifa ya afrika ambacho kimetajwa Mchana wa leo -
Mkufunzi mkuu wa timu hiyo Kwesi Appiah ameataja kikosi hicho leo jijini Accra alipokutana na waandishi wa habari .
Kama ilivyotegemewa Kiuongo wa , AC Milan Sulley Muntari bado yupo katika uangalizi wa baada ya kuanza mazoezi hivi karibuni .
Ni kweli kama mlivyosikia katika fununu kuwa Jordan Ayew ameachwa kwa sababu za kinidhamu na sio za kimpira .
Wachezaji hawa wawili tunawaacha katika kambi tutakayoweka kule Abu Dhabi Mwezi ujao na tutazama nini cha kufanya Tarehe 9 January 2013 ambapo ni tarehe ya Mwisho ya uwasilishaji vikosi vitakavyoshiriki michuano ya mataifa afrika .
Ghana ipo Kundi B Pamoja na DR Congo, Mali na Niger.
Kikosi Kamili
Makipa : Adam Kwarasey (Stromsgodset, Norway), Fatau Dauda (AshantiGold, Ghana), Daniel Adjei (Liberty Professionals, Ghana)
Mabeki : John Paintsil (Hapoel Tel-Aviv, Israel), Harrison Afful (Esperance, Tunisia), Mubarak Wakaso (Espanyol, Spain), Richard Kissi Boateng (Berekum Chelsea, Ghana), John Boye (Rennes, France), Jonathan Mensah (Evian, France), Isaac Vorsah (Red Bull Salzburg, Austria), Jerry Akaminko (Eskisehirspor, Turkey), Rashid Sumaila (Asante Kotoko, Ghana), Awal Mohammed (Maritzburg United, South Africa).
Viuongo : Andre Ayew (Marseille, France), Christian Atsu (FC Porto, Portugal), Anthony Annan (Osasuna, Spain), Derek Boateng (Dnipro, Ukraine), Emmanuel Agyemang Badu (Udinese, Italy), Kwadwo Asamoah (Juventus, Italy), Albert Adomah (Bristol City, England), Rabiu Mohammed (Evian, France)
Washambuliaji : Asamoah Gyan (Al Ain, UAE), Emmanuel Clottey (Esperance, Tunisia), Richmond Boakye Yiadom (Sassoulo, Italy), Yahaya Mohammed (Amidaus Professionals, Ghana)
No comments:
Post a Comment