Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmiliki na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short (kushoto kwa Rais), Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband (kulia kwake), Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Kagasheki, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fenella Mukangara, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim pamoja na maafisa wa Bodi ya Utalii bada y mkutano na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa mmiliki na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short huku Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband na Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan wakiangalia bada ya mkutano wa na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.
Uongozi huo wa Sunderlanda umesema kuwa baada ya kukutana na balozi wa Tanzania nchini humo na kuzungumza nae kuhusu swala la uwezekezaji Mwenyekiti wa klabu hiyo ameona bora waje kuonana na Viongozi wakuu wa nchi hasa baada ya Tanzania kudhamini ligi kuu ya Uingereza kwa kupitisha mabango mbalimbali yahusuyo utalii katika ligi hiyo ,
Aidha Rais kikwete amemsifu balozi wa Tanzania Nchini Uingereza kwa kazi walioyofanya na Waziri wa utalii Mh kagasheki kwani wamefanya kazi nzuri zaidi kipindi hiki .
Kwa upande mwingine baadhi ya wachezaji watapa mafunzo ya kwenda sunderland hasa wenye umri mdogo zaidi
Viongozi hao wa sunderland wamesema kitu kikubwa watakachofanya ni kuendeleza michezo katika sekta ya uongozi na na kutazama namna ya kutoa mafunzo kwa wachezaji na viongozi wa soka hasa katika swala la menejiment ambalo ndilo eneo lenye udhaifu zaidi katika michezo ,
kwa upande mwingine Rais alimwalika Mh Aden Rage mwenyekiti wa klabu ya soka simba ambao zamani walikuwa wakitumia hilo kabla ya kubadili kuitwa simba naibu waziri wa michezo fenela mukangara amesema kuwa hii ni faida ya kwanza ambayo tanzania inapata baada ya kutangaza katika ligi hiyo na waanaamini fursa zaidi zitajitokeza katika kutangaza katika ligi hyo .
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short huku Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband na Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan Ikulu jijijni Dar es salam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short, Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband, Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Kagasheki, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fenella Mukangara, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim pamoja na maafisa wa Bodi ya Utalii bada y mkutano na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.
No comments:
Post a Comment