HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

15 December 2012

Wachezaji wailaumu TFF sakata la Ngasa

Wakati baadhi ya wadau wa soka wakisikitishwa na kitendo cha winga Mrisho Ngassa kukacha kujiunga na timu ya El Merreikh ya Sudan, Chama cha Wachezaji Soka, SPUTANZA, kimelitupia lawama Shirikisho la Soka, TFF, kikidai ndiyo chanzo cha yote.

 Katibu Mkuu wa SPUTANZA, Said George, amesema jana kuwa kutokuwepo kwa elimu ya kutosha kuhusu suala la soka la kulipwa miongoni mwa wachezaji,  mawakala na viongozi wa kandanda nchini ndiko kumesababisha sakata la sasa la uhamisho wa Ngassa.

 George, nyota wa zamani wa timu za Coastal Union na Taifa Stars, amesema SPUTANZA waliliandikia barua TFF mwaka 2008 kutaka iitishe kikao cha uelimishaji kuhusu soka la kulipwa kwa wadau, lakini walipuuzwa.

 Amesema kutokana na ugeni kuhusu soka la kulipwa TFF ilipaswa kutoa elimu ya kutosha ili kuepusha "mambo ya aibu kama yanayotokea sasa", lakini hawakuungwa mkono hivyo inapaswa kulaumiwa.

 Ngassa amekataa kwenda kujiunga na El Mirreikh akidai kuwa uongozi wa klabu mama ya  Azam haukumshirikisha katika hatua za mwanzo za mauzo hayo, kama ambavyo ulimpeleka Simba kwa nguvu kwa mkopo.

 George aliongeza -- kama kungekuwa na elimu ya kutosha kwa wachezaji, viongozi na mawakala kusingekuwa na hali ya ubabaishaji kama ambavyo imekuwa ikitokea kwenye uhamisho na usajili wa wachezaji nchini.

Uongozi huo wa SPUTANZA umetoa kauli hiyo huku kukiwa na maoni tofauti kufuatia Ngassa kuchomoa usajili wa dola za Kimarekani 100,000 na kulipwa mshahara wa dola 4000 (sh. milioni 6) kwa mwezi pamoja na fedha ya ushawishi ya dola 50,000.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers