HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

11 January 2013

ETHIOPIA 2 TANZANIA 1





Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ethiopia uliochezwa leo (Januari 11, 2013) kwenye Uwanja wa

Addis Ababa hapa jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Mechi hiyo iliyochezeshwa na Bamlak Tesema wa Ethiopia ilikuwa ya kusisimua, hasa kutokana na timu zote kucheza kwa kasi

kwa muda wote. Wenyeji Ethiopia ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 13 lililofungwa na Fuad Ibrahim akiwa wastani wa hatua

sita kutoka kwa mlinda mlango Juma Kaseja wa Taifa Stars.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama kilivyokuwa cha kwanza, huku Ethiopia wakiwa wamefanya mabadiliko kwa wachezaji

watano. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 50 likifungwa na Mbwana Samata baada ya kumzidi maarifa beki

mmoja wa Ethiopia.

Bao la ushindi kwa Ethiopia lilifungwa kwa kichwa dakika ya 69 na mshambuliaji Shemelis Bekele aliyeingia kipindi cha pili

akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na winga Yossuf Sallah kutoka upande wa kushoto.

Taifa Stars inarejea nyumbani kesho (Jumamosi, Januari 12 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius

Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.

Taifa Stars: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Salum

Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mcha, mwinyi Kazimoto na Mbwana Samata.

Boniface Wambura
Media Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
Addis Ababa

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers