SIMBA SC
imetoka sare ya kufunga bao 1-1 na
Tusker ya Kenya katika mchezo wa Kundi A, Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja
wa Amaan mjini hapa.
Kwa matokeo
hayo, Tusker inaendelea kuongoza Kundi A, kwa piointi zake tatu sawa na Simba, lakini
mabingwa hao wa Kenya wana wastani mzuri zaidi wa mabao.
Hadi
mapumziko timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Simba wakitangulia
kupata bao dakika ya 18 mfungaji Haruna Moshi Shaaban, maarufu kama Boban au
Balotelli wa Bongo kabla ya Tusker kusawazisha dakika ya 39, mfungaji Khalid
Aucho.
Boban
alifunga bao tamu sana kwa ufundi wa hali juu akiwa amedhibitiwa na beki
ngongoti wa Tusker, Joseph Shikokoti na kuirukia pasi ya Ramadhan Chombo ‘Redondo’
kuitumbukiza nyavuni.
Baada ya
kufunga bao hilo, Boban aliangukia mkono na kuumia, hivyo hakushangilia bao
lake na moja kwa moja alianza kutibiwa na Daktari Cossmas Kapinga wa Simba.
Baada ya bao
hilo, Simba iliongeza mashambulizi langoni mwa Tusker na Boban alikaribia
kufunga tena dakika ya 30 kama si shuti lake kutoka nje sentimita chache.
Aucho
alifunga bao lake akiunganisha krosi ya Jeremiah Bright kutoka upande wa
kushoto wa Uwanja.
Baada ya
hapo, timu zilianza kushambuliana kwa zamu hadi refa Ramadhani Kibo alipopuliza
kipyenga cha kuhitimisha ngwe ya kwanza.
Kipindi cha
pili timu zote zilirudi vizuri na kucheza kwa umakini wa hali ya juu, jambo
ambalo lilisababisha dakika 90 zimalizike zikiwa zimefungana 1-1.
Katika mchezo
huo, kikosi cha Simba kilikuwa; William Mweta, Miraj Adam, Paul Ngalema, Shomary
Kapombe, Komabil Keita, Jonas Mkude, Haroun Athumani/MKussa Mudde75, Mwinyi
Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Ramadhan Chombo ‘Redondo’/Edward
Christopher dk 52.
Tusker FC; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng,
Jeremiah Bright/Humphrey Okoth, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho,
Edwin Manono/Benson Amanda, Justin Monda, Ismail Dunga/Michael Olunga, Jesse
Were na Robert Omon
binzubery blog
No comments:
Post a Comment