HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

25 January 2013

Wuuu Wuu Wuuu kwa Rage

 



Baadhi ya mashabiki wenye hasira wa Simba  walimzomea mwenyekiti wao Ismail Aden Rage na wengine kuondoka uwanjani wakati timu yao ilipowaacha nje wakali wao waliojifua Oman kwa takriban wiki mbili na kuchezesha ‘vitoto’ katika mechi ya kirafiki waliyolala 1-0 dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.

Simba walirejea jijini Dar es Salaam juzi jioni wakitokea Oman na matangazo ya mechi yao dhidi ya ‘Wasauzi’ yalidai kwamba watachezesha kikosi kamili cha kocha Mfaransa Patrick Liewig ili waonyeshe kile walichojifunza wakati wote walipokuwa wakijifua ‘umangani’.


Hata hivyo, kwa mshangao wa wengi waliofika uwanjani jana, ‘Wanamsimbazi’ walijaza wachezaji wao wa kikosi cha pili na kuzua malalamiko kutoka kwa baadhi ya mashabiki waliohisi kuwa wamepoteza pesa zao na muda kwa kuamini kuwa watashuhudia soka ‘tamu’ kutoka kwa nyota wao waliorejea kutoka Oman dhidi ya Leopards.


Hofu ya mashabiki wa Simba kuadhiriwa na Leopards ambao walishafungwa mara mbili katika mechi za awali walizocheza dhidi ya Yanga ilielekea kuwa ya kweli kwani wageni walisubiri dakika tatu tu kupata goli pekee la ushindi kupitia kwa beki Hassan Isihaka wa Simba aliyejifunga wakati akihaha kuzuia shuti la Mailase Make.


Baada ya bao hilo pekee, yosso wa Simba walicharuka na kufanya mashambulizi kadhaa kupitia kwa washambuliaji wao Ramadhani Singano na Ramadhani Ismail ambapo mojawapo ‘kali’ zaidi liliishia kugonga mwamba na mengine kuokolewa na kipa wa Leopards. Azindwin Maphaha.


Ushindi wa jana umewafanya Leopards wanaoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini walau kujipoza kwani kabla ya hapo walishakumbana na vipigo vya 3-2 na 2-1 kutoka kwa kikosi cha Yanga kilichorejea wiki iliyopita kikitokea kwenye kambi ya wiki mbili nchini Uturuki.


Kikosi kilichoanza Simba jana: Abuu Magube, William Luciana, Miraji Athuman, Ibrahim Hatibu, Hassan Kondo, Hassan Isiaka, Malisel Kaiza, Rashid Ismail, Ramadhani Singano, Said Ndeule na Emil Mgeta.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers