KAMATI
ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
inayoongozwa na Idd Mtiginjola imetupa maombi ya kufanyia marejeo
(review) uamuzi wake kama yalivyowasilishwa mbele yake na waombaji
watano.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za TFF, Dar es Salaam leo mchana
(Februari 18 mwaka huu), Mtiginjola ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo
amesema wamepitia Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF na kubaini
kuwa hakuna Ibara yoyote inayotoa fursa ya review kwa uamuzi ambao
wameshaufanya.
Amesema
Kanuni za Mwenendo wa Madai (CPC) katika mahakama za kawaida zinaruhusu
Hakimu aliyefanya uamuzi katika kesi kufanya marejeo, lakini katika
masuala ya mpira wa miguu hakuna fursa hiyo, hivyo hawawezi kujitungia
kitu kipya kwani kazi yao ni kufanya uamuzi kwa kutafsiri Katiba na
kanuni walizopewa na mamlaka ya uteuzi (TFF).
Waombaji
watano waliokuwa wakitaka Kamati hiyo ifanyie marejeo uamuzi wake
kutupa rufani zao ni Jamal Emil Malinzi aliyeenguliwa kugombea urais wa
TFF na Hamad Yahya aliyeondolewa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania
uenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).
Wengine
ambao waliomba kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Kanda zao
kwenye mabano ni Eliud Peter Mvella (Iringa na Mbeya), Farid Salim
Nahdi (Morogoro na Pwani) na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu)
No comments:
Post a Comment