Mgombea aliyeenguliwa na kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini TFF kuwania nafasi ya uongozi ndani ya shirikisho hilo Michael Richard Wambura, amesema hakushangazwa na maamuzi ya kamati ya uchaguzi iliyomuengua katika mchakato wa uchaguzi kwani alijua toka mapema kuwa maamuzi ya kamati hiyo yatakuwa hivyo.
Akiongea
na Rockersports Wambura amesema kwasasa anajipanga kukata rufaa katika
kamati huru ya rufaa ya uchaguzi ya shirikisho hilo.
Amesema kuwa hajui kuna nini ndani ya kamati hiyo kwani licha ya kusafishwa na kamati ya rufaa ya shirikisho hilohilo huko nyuma bado kamati ya uchaguzi inaendelea kumuhukumu kwa kutumia sababu zilezile za wakati ule ambazo kimsingi ni kamati ya rufaa ya wakati ule ambayo iliundwa na TFF yenyewe chini mwenyekiti wake Prof Fimbo Mgongo ilikwisha kumsafisha.
Amesema
kwa kuwa taratibu zinamtaka aende kwenye kamati ya rufaa baada ya
kuundwa kwa kamati huru ya rufaa, anajipanga kufanya hivyo.
Mapema hii leo taarifa ya kamati ya uchaguzi ya TFF iliyotolewa na mwenyekiti wake Deogratius Lyatro ilitangaza kumuengua Michael Richard Wambura kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF kwababu zilizo ainishwa kuwa hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni
za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kuwa Ndg. Michael Wambura alifungua
kesi ya madai namba 100 ya 2010 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
Dar es salaam dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba akiwa ni mwanachama
wa Klabu ya Simba, kinyume na Katiba ya Klabu ya Simba.
Kwa kufanya hivyo kamati hiyo imesema Michael Wambura alivunja Katiba ya Klabu ya Simba, alikiuka Katiba ya TFF na Katiba ya FIFA na hivyo kumuengua katika kinyanganyiro hicho.
No comments:
Post a Comment