Upimaji
uzito katika mapambano mawili ya IBF yanayofanyika katika majiji ya
Johannesburg na Tunis umefanyika vizuri leo.
Mapambano
haya yaliyopewa jina la “Barabara ya kutoka Cape Town mpaka Cairo kwa
IBF” kutokana na majiji haya kukaa moja kusini na lingine kaskazini mwa
Afrika, yanafanyika wakati IBF ikijipambanua vyema katika bara la Afrika,
Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.
Kusini
mwa Afrika, leo imeshughudia mabaondia mawili wanaopambania ubingwa wa dunia
kwa vijana walio chini ya miaka 25 wakipima uzito mbele ya mashirika mbalimbali
ya habari ya ndani na nje ya Afrika ya Kusini.
Illunga Makabu kutoka Jamhuri ay Watu wa Kongo (DRC)
alipima uzito kumkabili Gogota Gorgiladze wa Georgia. Upimaji huo ulifanyika
katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa ulio katika hotel ya nyota tano ya Emperors
Palace iliyoko katika jiji la Johannesburg!
Rodney
Berman mtu anayeheshimika kwa kuwa promota wa kwanza kuandaa pambano la IBF la
dunia katika bara la Afrika mwaka 1990, ndiye anayepromoti pambano hili!
Tayari
wadau na mashabiki wa ngumi kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika zikiwamo Namibia,
Zambia, Msumbiji, Zimbabwe na Tanzania wameshawasili nchini Afrika ya Kusini
tayari kuangalia mpambano huo. Wengine walibaki Afrika ya Kusini wakati wa
mashindano ya kombe la Afrika yaliyomalizika wiki iliyoita.
Msimamazi
mkuu wa mpambano huu ni Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na
Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi aliyesimama pichani na mabondia Gogita
Gorgiladze (kushoto) na Ilunga Makabu (kulia)
Kaskazini mwa Afrika,
Bondia
ambaye ameshajizolea sifa kemkem Ayoub Nefzi wa Tunisia anayeishi nchini
Belgium atapigana na bondia Ishmael Tetteh kutoka nchi ya Ghana kugombea
ubingwa wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na
Mashariki ya Kati (IBF AMEPG) katika uzito wa Light Middle.
Mpambano
huo uliopewa jina la “Uzuri wa Jasmine” kutokana na jina hilo kutumika
katika mapinduzi yaliyomwondoa Rais wa zamani wa Tunisia Ben Ali unafanyika
wakati Ayoub Nefzi akijiandaa kugombea mkanda wa juu wa IBF wa mabara
mwezi wa tatu nchini Belgium.
Mabondia
wote wawili wanatagemea kuonyesha moto mkali katika mpambano ambao tayari
mashabiki wa ngumi kutoka katika nchi za Nigeria, Ghana, Libya, Misri, Algeria
tayari wameshawasili nchini Tunisia kuangalia mpambano huo!
Tunisia
inasifika kama nchi iliyowahi kutoa viongozi wengi wa mchezo wa ngumi katika
bara la Afrika.
Imetolewa na:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA
(IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment