ALIYEKUWA katibu mkuu FAT (sasa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) Michael Wambura, kwa mara nyingine amekusudia kwenda mahakamani
iwapo uongozi wa TFF utafanya uchjaguzi wa viongozi kwa kutumia kanuni mpya.
Wambura amesema leo kwamba amefikia uamuzi huo
baada ya kubaini kufanyika kwa njama ili uchaguzi usifanyike ama uharibike na
viongozi waliopo sasa waendelee kuwepo madarakani.
Amesema katiba iliyotumika kuitisha
uchaguzi huo ni batili kwa kuwa mabadiliko yake hayakufuata utaratibu wa kikatiba
kwani hakuna mkutano mkuu wowote wa TFF uliokaa kupitisha mabadiliko hayo.
“TFF imempotosha msajili wa vyama kupitia
ibara ya 76 ya katiba ya TFF ya kuwa Mkutano mkuu wa TFF ulikutana Desemba 15,
2012 kufanya mabadiliko hayo huku ikijua sio kweli, ninapenda kuitahadharisha
TFF hili sio suala mchezo ni swala la kisheria, hibyo kwa mujibu wa sheria za
nchi mwenye mamlaka ya kutafsiri sheria (katiba) ni mahakama hivyo ushauri
wangu kwa TFF ili kuondoa uwezekano wa mkono wa sheria kuingia hawana budi
kufuata haya,’alisema
Mosi, Wambura ametoa pendekezo la
kusimamisha matumizi ya katiba hiyo mara moja kwani sio halali kuondoa
uwezekano wa kutafutwa haki kwenye mahakama za kiraia.
Pili Wambura ameitaka TFF kuyafuta maamuzi
yote na kuivunja kamati ya rufaa ya uchaguzi inayoongozwa na Iddi Mtinginjola
an ili matakwa ya kikatiba ya uchaguzi yatimie rufani zote zirudishwe kwenye
kamati ya rufaa kama katiba halali inavyotaka ili kukamilisha mchakato wa
uchaguzi.
Tatu, maamuzi yakliyofanywa na kamati ya
uchaguzi chini ya Lyato (Deo-Mwenyekiti wa kamati) yaheshimiwe na kama kuna
wasioridhika wakate rufgaa kamati ya rufaa ya TFF, pamoja na kuwa maamuzi ya
Lyatto hayana maamuzi ya moja kwa moja nay eye lakini ataweka misingi bora ya
kikatiba.
Akifafanua zaidi, Wambura alisema kwa
mujibu wa katiba mpya ambayo yeye anaiita sio halali ibara ya 76 katiba hiyo
imeanza kutumika desemba 15,2012 na kanuni za uchaguzi zimeanza kutumika
januari 7, 2013 ambapo kanuni hizo na katiba yake ndio zilizotumika kuitisha
uchaguzi mkuu.
“Baada ya kupitisha katiba mpya na kuanza
kutumika TFF ilipaswa kuunda kamati mpya ya uchaguzi, kwa mujibu wa katiba ya
TFF ibara ya 49 (4) mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi anapaswa kuwa na taaluma
ya sheria sifa ambayo Lyatto hana na
hivyo ushiriki wake kuwa kinyume na katiba ya TFF, hali ianyoufanya uchaguzi
wake kuwa batili na unapaswa kufutwa na kuteua kamati mpya ili mchakato uanze
upya hivyo kuchelewesha kupatikana kwa viongozi wapya wa TFF,”alisema
“Kanuniu hutengenezwa ili kuwezesha
utekelezaji wa katiba husika hivyo katiba hupitishwa na kusajiliwa kwanza na
baadaye hutungwa kanuni, cha kushangaza kanuni za uchaguzi za TFF zilipitishwa
na kusainiwa na Januari 7, 2013 wakati
katiba ya TFF ilisajiliwa na kugongwa muhuri wa msajili Januaro 10 siku tatu
baada ya kanuni kusasiniwa.
“Swala linakuja kanuni hizi zilitungwa kwa
mujibu wa katiba batili kisheria, ninaishauri TFF ili kuondoa uwezekano wa
kuingiza TFF kwenye mgogoro wa kisheria, uamuzi wa busara wa kuachana na katiba
batili ni muhimu kwa maendeleo ya soka Tanzania kwa kusimamisha matumizi ya
katiba mpya batili ya TFF na matokeo ya maamuzi yote yanatokana na katiba
hiyo,”alisema
Awali, Wambura ambaye alikuwa akigombea
nafasi ya makamu wa Rais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika februari 24, jina
lake lilienguliwa kutokana na sababu kadhaa ikiwemo suala la uadilifu.
Alisema matarajio yake ya kuwania nafasi
hiyo yalianza kuingia dosari kwa mara ya nne
tangu 2008 katika chaguyzi mbalimbali ambazo TFF ina maslahi nazo ambapo
jina klake liliondolewa na kamati ya uchaguzi kwa sababu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment