Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa
Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) uliochaguliwa
katika uchaguzi uliofanyika juzi (Machi 16 mwaka huu) mjini Dodoma.
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TAFCA walivyo na imani kubwa kwao katika
kusimamia taaluma ya ukocha nchini.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TAFCA
chini ya uenyekiti wa Oscar Don Koroso aliyeibuka mshindi kwa kura zote
za ndiyo baada ya kukosa mpinzani.
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha
shughuli za mpira wa miguu kwa kuzingatia katiba ya TAFCA pamoja na
vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA chini ya Ramadhan
Mambosasa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo
unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Safu
nzima ya uongozi wa TAFCA iliyochaguliwa inaundwa na Dk. Oscar Dan
Koroso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti), Michael Bundala
(Katibu Mkuu), Gabriel Gunda (Katibu Msaidizi), Dismas Haonga
(Mhazini), Wilfred Kidao (mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF).
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa ni Jemedari Saidi, George Komba na Magoma Rugora.
No comments:
Post a Comment