Michuano ya kufuzu kwa fainali ya kombe la mataifa
bingwa barani Afrika ACN, mwaka wa 2015, itachezwa kwa muda wa miezi
mitatu pekee mwaka Ujao.
Tangazo hilo limetolewa na shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika CAF.
Uamuzi
huo sasa unamaanisha mechi mia moja na arubaini na nne, zinazojumuisha
timu 48, katika makundi 12 ya timu nne kila mmoja itachezwa kati ya
Septemba na Novemba mwaka ujao.
Ratiba hiyo mpya, imepangwa ili kuwiana na ratiba ya mechi za kimataifa ya shirikisho la mchezo huo duniani FIFA.
Vile vile mashindano hayo hayatakuwa na nafasi mwaka wa 2014, kabla ya fainali za kombe la dunia itakayoandliwa nchini Brazil.
Hii ni mara ya kwanza kwa fainali hizo,
kuandaliwa nje ya mwaka ambao fainali za kombe la dunia kufanyika, tangu
ilipoamuliwa kuwa mashindano hayo yafanyike mwaka mmoja kabla na baada
ya fainali za kombe la dunia.
Na kutokana na matatizo ya usafiri barani
Afrika, ratiba hiyo mpya huenda ikakumbwa na matatizo hasa kutoka
mashariki hadi magharibi mwa Afrika.
Matatizo ya fedha
Wachezaji wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Timu itacheza mechi moja mwishoni mwa wiki na
kupumzika kwa siku mbili kabla ya kucheza mechi nyingine kuambatana na
ratiba ya FIFA.
Wachezaji wanaoshiriki ligi za kulipwa ni sharti waruhusiwe na vilabu vyao kuaklisha mataifa yao katika mechi hizo.
Mechi hizo zimepangiwa kuchezwa kati ya tarehe
Moja hadi Tisa Septemba, kisha tarehe Sita hadi tarehe Kumi na Nne
Oktoba na mechi za mwisho zitachezwa kuanzia tarehe Kumi hadi Kumi na
Nane Novemba.
Rais wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Namibia, John Muinjo, anaamini ratiba hiyo mpya itawapa changamoto nyingi.
Amesema kucheza mechi sita za kimataifa kwa muda wa miezi mitatu itakuwa ngumu sana na hatari hata kwa afya ya wachezaji.
Aidha amesema kutokana na matatizo wa fedha,
wasimamizi wa soka katika nchi kadhaa huenda wakashindwa kuwasafirisha
wachezaji wao kutoka nchi moja hadi nyingine kwa muda mfupi.
Baada ya kukamilika kwa hatua ya makundi,
washindi wa kila kundi watajumuika na timu zingine tatu zilizoandikisha
matokeo mema zaidi katika makundi yao kufuzu kwa kwa hatua ya mwisho ya
kufuzu ambayo itaandliwa nchini Morocco kati ya mwezi Julai na Agosti
mwaka wa 2015.
No comments:
Post a Comment