Na Andrew Chale 0719 07 63 76
MWANAMUZIKI nguli wa bongo na kiongozi wa yenye mvuto nchini
bendi ya ‘Machozi’, Judith Wambura (
Lady JayDee) au Jide ama #Teamaanaconda#, anatarajia kuripoti Mahakama ya Kinondoni
siku ya Jumatatu Mei 13, kufuatia kufikishiwa kwa taarifa hizo Gadna G Habash ‘Captain’
ambaye ni Meneja na mumwe wa Lady Jay Dee.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mchana wa leo, Gadna
alisema ni kweli wamepata taarifa za kutaarifiwa kwa Lady Jay Dee kufika
Mahakama ya Kinondoni, siku ya Jumatatu.
“Ni kweli tumepata wito na Mahakama ya Kinondoni, Hii ni kufuatia kwa jana kufika watu ambao walijielezea kuwa wanatoka
Mahakama hiyo na walikuja na barua ya kumkabidhi Lady Jay Dee mwenyewe hata
hivyo hawakumkuta” alisema Gadna.
Aliendelea kueleza kuwa, hata alipowaeleza watu hao
wamkabidhi yeye hiyo barua watu hao walisema ilikuwa si lahisi zaidi alitakiwa
akabidhiwe mlengwa, hivyo kumueleza kuwa wito wa kufika mahakamani siku ya
Jumatatu, na aliwakubalia kwa hilo.
Hata hivyo, Gadna alisema hajajua Lady Jay Dee anaitiwa nini
na kwa sababu ya nani zaidi amemwelezea na amesema watatekeleza wito huo wa
kufuka Jumatatu Mahakamani hapo.
Aidha,
kupitia kwenye ukurasa wake wa Kijamii wa facebook, Lady Jay Dee
aliandika: “Ratiba ya Usiku wa leo, ni Machozi Band, kama kawaida, ila
ratiba ya
Jumatatu natakiwa Mahakama ya Kinondoni..Taarifa zaidi zitafuata nikijua
kinachoendelea...” aliandika Jide kwenye
ukurasa huo ambao mpaka hatua ya mwindishi anatembelea ‘post’ hiyo
ilikuwa na
maoni mengi ambayo watu mbalimbali walipata kuchangia.
Maoni hayo yanayokaribia zaidi ya 558 na, ‘Like’ zaidi ya
756 na ‘Share’ zaidi ya 20, ambapo wengi
wao wameweza kumuhusisha moja kwa moja na Mkurugenzi wa Clouds Fm, Ruge Mutahaba
kuwa ndie aliyefanya hivyo.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali na moja ya gazeti hivi
karibuni ilimnukuu Ruge kuwa amejiandaa kuchukua hatua ikiwemo ya kisheria dhidi ya Lady Jay Dee
baada ya kumsema kupitia kwenye mitandao ya kijamii.
**
Aidha, katika kuelekea shoo yake ya Miaka 13 ya Lady JayDee,
amemtangaza rasmi msanii machachali wa bongofleva, Juma Nature.
Jide alisema Nature ameongezeka katika list ya wasanii
watakaokuwepo kushiriki miaka 13 ambapo
ataungana na wasanii wengine wengi siku hiyo
ambapo tayari tiketi zimeanza kuuzwa. “Naomba mujitokeze kwa wingi na
tiketi zinapatikana karibu sehemu zote ikiwemo Shear Illusions Mlimani City,
City Sports Lounge Mjini Posta, BM Salon Kinondoni, American Nails n Hair Salon,
bila kusahau Nyumbani Lounge mahala
patakapofanyika shoo hiyo
No comments:
Post a Comment