Hali ya ati ati imekumba timu ya taifa ya soka ya
Ethiopia huku kukiwa na wasiwasi ikiwa itaweza kuendelea na safari ya
kuwania nafasi ya kufuzu kushiriki kombe la dunia nchini Barzil mwaka
ujao au la. Hii ni baada ya shirikisho la soka duniani FIFA kuwachukulia
hatua za kinidhani wachezaji wa kikosi hicho Jumapili.
Mapema hapo jana , Ethiopia waliicharaza Afrika
Kusini mabao mawili kwa moja mjini Addis Ababa na kujipatia nafasi nzuri
katika kinyang'anyiro cha kufuzu kwa kombe la dunia.
Hata hivyo, kufuzu kwa Ethiopia
kunahojiwa baada ya tuhuma kuwa walimshirikisha mchezaji asiyefaa kwenye
mechi hiyo ambapo walishinda mabao 2-1wakati walipokuwa wanamenyana na
Botswana tarahe nane mwezi Juni. Ikiwa Ethiopia watapatwa na hatia
huenda wakapoteza mechi yao waliyocheza dhidi ya Botswana.
FIFA pia inachunguza kikosi cha Togo na kile cha Equatorial Guinea kwa kosa sawa na hilo.
Ikiwa timu hizo zitapatikana na hatia huenda zikaathiriwa vibaya katika kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao Brazil.
Kesi dhidi ya Ethiopia inatia wasiwasi kwani
ikiwa watapatikana na hatia huenda ndoto yao ya kushiriki kombe la dunia
mwaka ujao ikaambulia patupu huku Afrika Kusini waliokuwa wenyeji wa
kombe la dunia mwaka 2010, wakashiriki kwa mara nyingine.
Kwa sasa Ethiopia wako na pointi tano mbele ya
Afrika Kusini katika kundi A na Afrika Kusini itakuwa tu na ponti mbili
nyuma ikiwa Ethiopia watakubali Bostwana kutwaa ushindi kwa kosa lao la
kumchezesha mchezaji asiyefaa au asiyestahili kucheza.
Tangazo hilo la FIFA, halitaipa tu uhai timu ya
Afrika Kusini bali wachezaji wa Cameroon na Cape Verde.Cameroon
walicharazwa mabao mawili kwa nunge na Togo lakini timu hiyo huenda nayo
ikapata pointi tatu zengine ikiwa Togio watapatikana na hatia.
No comments:
Post a Comment