Timu ya soka ya Gor Mahia ya kenya imekubali kuchukua nafasi ya mabingwa wa kenya Tusker katika mashindano ya CECAFA Kagame
Cup ambayo yanatarajia kufanyika wiki chache zijazo .
Katibu mkuu wa timu hiyo George Bwana aliuambia mtandao moja wa www.starAfrica.com kuwa timu yake ipo tayari kuchukua nafasi hiyo .
Tusker imejitioa katika mashindano hayo, kwa kile kinachodaiwa kuwa kutokuwa na uhakika wa usalama . Wameandika Barua kwa shirikisho la soka la kenya (FKF) ambayo kopi ya yake ilielekezwa kwa katibu mkuu wa Cecafa ikisema hawako tayari kushiriki michuano hiyo kwasababu hakuna uhakika wa ulinzi .
Aidha kwa upande wa katibu mkuu wa , Cecafa Nicholas Musonye ambaye anakaa Kenya amesema kuwa Tusker itashughurikiwa kisheria na kinidhamu na kupigwa faini kwa kujitoa katika mashindano .
Bwana,anaongeza kwa kusema kamati ya utendaji imekutana na kuamua kuwa watapeleka timu ya vijana katika kuikuza timu yao ..amesema mashindano hayo yatawasaidia kujua ntimu yao ya vijana imefika hatua gani .
“Tulifanya mkutano na viongozi wetu na kulizungumzia jambo hili na tumekubaliana kuwa klabu itakubali mwaliko wa CECAFA
kushiriki mashindano hayo .
Gor Mahia ilimaliza nyuma ya Tusker Mwaka 2012 ikiwa na alama 59 baada ya kucheza mechi 30 .
Wakati huo huo,Dirisha la usajili linaendelea ,na klabu hiyo imewaachia Ali Abondo na Moses Otieno ili kuleta nafasi kwa wachezaji wapya .
Japokuwa ,makamu wa rais wa kwanza Faiz Magak amekataa kuwa wameachia huru wachezaji hao Abondo bado ana kandarasi ya mwaka mmoja lakini amekubali kuwa wamemwacha Otieno.
No comments:
Post a Comment