Javier Mascherano ameomba radhi kwa kutandikwa kadi nyekundu baada ya kumpiga mwendesha gari ya kutolea majeruhi kiwanjani katika mchezo wa kufuzu kombe la dunia dhidi ya Ecuador.
Kiungo huyo wa
Barcelona ,ambaye aliwahi kuchezea Liverpool na West Ham,alitolewa baada ya kumpiga dereva wa gari ya kuondolea wachezaji majeruhi kiwanjani katika dakika ya 87th.
Mascherano, ambaye alikuwa nahodha wa timu hiyo kwa usiku huo,Baadae alisema kuwa: 'Hakuna mtu anayependa fujo nchini kwetu nilifanya makosa naona aibu kwa kufanya vile .
Mwendesha gari alikuwa anakwenda kwa kasi kubwa sana ilikuwa bado kidogo nidondoke.Nilimkanya (Dereva)lakini alidharau, lakini nilichofanya hakikuwa kitendo cha haki .
‘Nina elewa umuhimu wa mimi kuomba radhi . Nimefedheheshwa ,na kwa masikitiko nimeomba radhi.’
kwenye mtandao wa Twitter,: 'Nakiri nimefanya kitendo kibaya,hakielezeki.
Baada ya kuumia , Mwendesha gari alikuja kunichukua kama sheria inavyotaka .
Japokuwa Kiungo huyo, alianzisha fujo kama alivyokuwa akionekana kwenye Tv .na picha za ruinga zilionyesha , Mascherano akiwa anapiga makelele kwa wahudumu wa huduma ya kwanza .
No comments:
Post a Comment