Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, amewashangaa
baadhi ya mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wanaolaumu kuachwa kwa
mlinda mlango mkongwe Juma Kaseja kwenye usajili wa wachezaji wa timu
hiyo kwa msimu ujao.
Rage amesema kuachwa kwa mchezaji kwenye timu ni jambo la kawaida na kusisitiza kama viongozi hawatolizungumzia tena suala la kipa huyo.
"Hivi kuna ajabu gani mchezaji kuachwa?" aliuliza Rage ambaye pia ni Mbunge.
"Maamuzi yaliyotolewa ndio hayo sasa kwa nini kila wakati watu wanazungumzia jambo hili la kuachwa kwa Kaseja.
"Mimi nafikiri tumuache apumzike na aamue mambo yake... tunakuwa hatumtendei haki kumzungumzia kila wakati."
Alisema kuwa uongozi umeamua kuachana na mlinda mlango huyo na umempa nafasi ya kuamua anachotaka kufanya hivyo suala la golikipa huyo wamelifunga.
Rage amesema hakuna ajabu kuachwa kwa mchezaji huyo kwa sababu mkataba wake wa kuichezea timu hiyo umemalizika.
Kuachwa kwa Kaseja ambaye pia ni mlinda mlango namba moja wa timu ya taifa kumelalamikiwa na baadhi ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo.
Baadhi ya wanachama wanasema uongozi haukumtendea haki golikipa huyo aliyeichezea Simba kwa miaka inayotenganishwa na msimu mmoja aliohamia Yanga kabla ya kurudi Msimabzi kwa kuwa bado ana uwezo mkubwa.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini kwa sababu si msemaji wa masuala ya Simba aliiambia Nipashe golikipa huyo ameachwa kwa mapendekezo ya kamati ya ufundi na kocha Abdallah Kibadeni.
Kutemwa kwa Kaseja kunatoa nafasi kwa golikipa namba mbili wa klabu hiyo Mganda Abel Dhahira na mlinda mlango aliyesajiliwa kutoka Kagera Sugar Andrew Ntala kurithi namba ya Kaseja msimu ujao wa ligi kuu utakapoanza.
Kaseja alijiunga na Simba 2003 akitokea Moro United na ndiye aliyepangua penalti iliyoiwezesha timu hiyo kuivua ubingwa wa Afrika Zamalek ya Misri mwaka huo na kucheza kwa mara ya kwanza na ya mwisho Ligi ya Klabu Bingwa chini ya kocha James Siang'a.

No comments:
Post a Comment