Soka Soka Soka!!! kila kukicha Simba na yanga zinaibua mambo mapya
hasa katika maswala ya kiundeshaji wa Timu hizi haziishi lawama kwa tff
Viongozi wa Timu Hizo hawaishi kugombana Mipango isiyokwisha kila kukicha kama
Hauamini Ngoja nikueleze-: Asilimia kubwa ya wachezaji wanaosajiriwa Simba na yanga ni kwa kukomoana sikutajii majina ya wachezaji hao kwani kwa hawana nafasi kwa sababu sioni kiwango chochote wanachokionyesha zaidi ya kuruka ruka kiwanjani .
Leo nataka kuwaeleza mchawi wa soka la Tanzania! hivi karibuni Rais wa Tff Leodgar Chila Tenga alisema kuwa wachezaji wengi wanaocheza timu ya taifa hasa wadogo hawajazinduliwa katika vilabu vyao wengi wamechukuliwa katika mashindano yanadhaminiwa na baadhi ya makampuni ya yanajitolea kuendesha soka la vijana chini ya miaka ishirini. sasa ngoja niende kwenye hoja ya msingi simba na yanga hazina shule za soka na kama zipo naomba wanionyeshe zikiwa na vitu vifuatavyo vifaa vya kufundishia eneo lilipo hiyo shule mara kadhaa makocha wakigeni huwa wanapata Tabu sana kuchagua timu ya taifa kwa sababu kubwa ya wachezaji hao kupanda na kushuka kwa uwezo wao kiwanjani Utafikili Lift za ghorofani kwani kuna baadhi ya mambo hawakupitia hata kidogo .
Usajiri wa simba na yanga siku zote huwa haufuati ufundi hata kidogo ni genge la watu ambao ukaa tu nakuamua leo tumsajiri fulani na kuweka siasa nyingi utafikili wanagombania jimbo sababu kubwa huwa hawatazami mambo haya ya soka kiufundi. kwa mfano katika miaka mitatu iliyopita jumla ya makocha zaidi tisa hivi wamefundisha vilabu hivi wengine wakifungashiwa vilago pindi timu inapokuwa na matokeo mabaya simba na yanga ni timu ambazo hazikataki kufungwa hata kama hawajui wao wanataka washinde zikifungwa kocha hafai .
Tawala za timu hizi ndipo penye mkasa mkubwa Tawala za timu huwa zinaenda mlama pindi simba ikifungwa na yanga au yanga ikifungwa na simba hapa ni kanakwamba timu hizi zimeandikiwa katika katiba zao kuwa ni Marufuku kufungwa na Mpinzani wake kwa njia yoyote ile ,
katika mpira wa miguu mambo hayaendi namna hiyo kila siku hutaskia katika katika vyombo vya habari majigambo ya kugombania wachezaji utafikili Tanzania inawachezaji wawili au watatu ambao ndio bora kuliko wote Dunuani.
Sitaki kutoa Miafano ya Nchi zilizo endelea kisoka Duniani mifano yangu ipo hapa hapa afrika Naanza na Azam Fc timu inayomilikwa na Mfanya biashara maarufu Tanzania Said Bakhresa huyu alichofanya mungu alimjaria uwezo lakini akaamua kuwaachia watu wanaojua ufundi katika soka ndio waongoze timu na yeye kukaa Pembeni siku wahi kuiskia hata siku moja sauti ya Mzee huyu kwenye radio au Tv ikipiga makelele kuhusu usajiri Ukiskia habari yoyote kutoka Azam ni sauti ya Jaffar Iddy Ndiye mtu anayeweza kuzungumza kuhusu timu hiyo.
Lakini simba na yanga kila mtu ni mzungumzaji ndio maana zi nakuwa hazina mipango sasa naomba mnisaidie kuna tofauti gani katika timu hizi mbili na soko la samaki Feri au kariakoo kama umewahi kupita kariakoo mchana utakutana na kelele sizokuwa na mpangilio maalumu honi za magari ,mashine za kusagia juisi,Kelele za jenereta, kelele za wafanya biashara ndogo ndogo muziki wenye sauti kubwa kelele za watu zilizo changanyikana na Matusi ya Nguoni vibaka Tabia hizi za kariako ndizo utakazo zikuta simba na yanga lakini sishangai sana kwa sababu hata zenyewe zipo kariakoo kwani zinaweza kuwa ni tabia za kiasili kwao.
Sasa tazama sifa za kariakoo na sifa hizi ninazo zitaja jambo la kwanza kugombania wachezaji bila kujari uwezo wao hupigizana makelele mwezi mzima kuhusu usajiri tu fitna ziszo na msingi ,vurugu za makundi katika vilabu hivyo viwili vya kugombania nani aongoze timu hiyo mapinduzi ya mara kwa mara yasiyo kwisha kufukuzwa makocha kuliko kithiri kiasi kwamba hata makocha wa timu hizo wanakuja kutoka nje wangejua kuhusu historia za timu husika wallah wasingethubutu hata kusaini kandarsi za muda mfupi,
Je niambieni wakati mwingine ni kheri ukawa na tabia za mbuzi kuliko kulio kuwa na tabia za simba na yanga ambazo hata mbwa hawezi kuwa nazo .
Usajiri wa timu wachezaji wengi wanaosajiriwa kwa pesa nyingi huwa hawachezaji kwenye tinu zao za taifa nchi wanazotoka achana na hilo tangu timu hizo zimeanza kusajiri hakuna hata siku moja zimefanikiwa kucheza robo fainali ya afrika au kombe la shirikisho sasa utasema una timu hapo? mimi leo naamua kuwaeleza wazi kuwa simba na yanga kamwe hazitoweza kuchukua ubingwa wa afrika labda nabii Isah au yesu arudi.
kama simba iliweza kufungwa mbele ya mwinyi unategemea nini yote ni kwa sababu ya mipango mibovu ya soka sioni tofauti kati ya Genge la wahuni na timu hizi .
Azam Leo wanakaribia kuanzisha Runinga yao ya kulipia simba na yanga hata radio ya mita kumi hawana nina jambo kuu CAG akague pesa za usajiri wa timu hizi kwa sababu hazina chanzo cha mapato cha uhakika zaidi ya pesa za mlangoni je wanapata wapi pesa hizi ? wanafanya Biashara gani kiasi kwamba wawe wanatoa mamailiano ya shilingi kila Dirsiha la usajiri ilinapofunguliwa?
Japo kuwa wanapata uzamini wa kilimanjaro kampuni inayo zalisha vinywaji kadhaa vya maji ya dhahabu hapa ndipo soka inapokufa kabisaa kwani vilabi hivi vinapewa nguvu nyingi sana kuuwa sisimizi huku timu nyingine zikiachwa hoi Bin TaaBan, sasa hapo huwezi kupata Ligi bora hata kidogo ni Ndoto wazamini siwezi kuwalaumu lakini na wao wanachangia kuuwa soka la Tanzania.
hatuwezi kufika mbali kwa mfumo huo jamani tubadilike yapo mambo mengi sana ambayo mfumo wa uongozi wa timu hizo haujafanikiwa iko wapi simba Tv zikowapi harakati za kujenga Kiwanja Eti wanafurahia kuwekewa sheria kuwa timu lazima iwe na kiwanja hio ni aibu huwezi kulazimishwa kulima kwa njaa yako mwenyewe simba na yanga zilikwisha feri mtihani wa kuingia shule ya vidudu yaani chekecheea itakuwa chuo kikuu .
No comments:
Post a Comment