HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

16 July 2013

VIWANJA HIVI VYA SOKA VINAKALIBIA KUPATA UGONJWA WA SARATANI YAANI CANCER !

 
Jamhuri Morogoro
Mpenzi msomaji Leo nimeona tuvitazame japo kwa uchache viwanja vyetu vya soka Nchini Tanzania 
Kiwanja unachokiona juu pichani ni uwanja wa Jamhuri Morogoro ambao haumilikiwi na Shirikisho la soka la Tanzania  Tff bila shaka inaweza kuwa Manispaa na unaposema manispaa tunamaana ya serikali ambayo imeongozwa na Chama cha Mapinduzi Nia ya hapa sio kukisema chama cha mapinduzi hapana , ni kuuambia umma kuwa tufute kwanza mawazo ya kucheza kombe la dunia na badala yake tutengeneze viwanja vyetu vya soka .
Kifupi nimekuwa nikifikiri sana kuhusu mustakbari wa michezo na  soka la Tanzania kwa weli ukiuondoa uwanja wa Taifa ule mpya na uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam viwanja vingine vinavyofuata kwa ubora katika ardhi ya Tanzania vinapumulia mashine .
Kiwanja unachokiona hapo  juu pichani ni  mji kasoro Bahari kwa maana ya Morogoro ukitazama hari yake ni ya kusikitisha tu hasa sehemu ndogo inayoonekana pichani sasa hapa bado ligi kuu ya Tanzania hapa nafasi ya kuonekana katika Ruininga kubwa Duniani kwa kweli kwa kiwanja hiki Tanzania kufanikiwa kimataifa Labda yesu au nabii Issah harudi kutoka Mbinguni sina haja ya kuelezea sana sehemu kama choo ,vyumba vya kubadilishia nguo ,chumba cha kufanyia mkutano na waandishi wa habari kwa hari hii haina haja ya kupaona ni kichechefu.
Jukwaa lenye unaona lilivyo ni full bati sasa ubora wa soka hutapatikana vp hapo
 

Hiki  pichani ni kiwanja cha Sokoine Mbeya uwanja huu haufanani kabisa na jina uliopewa kwani mwenye jina hili alikuwa mfanyakazi hodari katika cheo cha uwaziri mkuu wa jamhuri ya muungano kiukweli hapa waliamua kumdhalilisha tu Moringe kwani kiwanja hiki ni  sehemu yenye Kaunafuu ni ya kuchezea soka tu ambayo na yenyewe haina ubora huo kwa picha hii ilipigwa miezi mitano iliyopita sidhani kama utakuwa umerekebishwa  kwani kwa kifupi uwanja huu  hauna choo na hauna sehemu kuu za mahitaji ya binadamu hata kidogo kifupi ngoja niseme hivi hata mbwa hawezi kuishi kwenye kiwanja hiki atapata ugonjwa saratani ya mwili

          Hayati Moringe sokoine ni moja kati ya Viongozi shupavu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini siwezi kuamini kama uwanja huu unabeba jina kama hilo la kihistoria Tanzania ukitazama vizuri picha hiyo  ya Nyasi zipo hadi sehemu ya kuingilia kiwanjani Yaa Rabi sitaki kusema sana naogopa kukufuru unamilikiwa na nani uwanja huu jamani ?


 
Hawa pichani ni wananchi wa mkoa wa Ruvuma katika uwanja wa Majimaji wilaya ya songea wakisikiliza kampeni ya chama cha mapinduzi yaliopo kiwanjani hapa hayatofautiani kabisa na uwanja wa Sokoine Mbeya
  
Uwanja wa Kaitaba
Tehe teh Hapo ni kwa ndugu zangu wahaya kaitaba hao ni wachezaji wa yanga wakiwa wamekaa katika becnhi wakitazama mchezo kati ya timu yao na Kagera Sugar kuna  haja ya kukwambia sehenu nyingine zilivyo kama bechi tu liko na hari hiyo hilo ni Benchi kweli sio masihara 
 
Pengine swali :Uwanja uliopewa jina la kiongozi wa serikali ya awamu ya pili umechoka na kuchakaa hata kabla haujakamilika.
Naogopa kuuita gofu. Fremu za maduka zinazouzunguka ambazo zingeweza kuuingizia mapato ,sasa zinatumika kama vyoo hivyo kupigwa makufuli. Mmh.? Mhusika hebu  kideo hapa chini  kidogo
 
Uwanja wa ushirika moshi kwani timu ilikwsiha kufa sio kushuka daraja ilikwisha kufa siskii tena hapa ndipo na kiwanja nafikiri kitakuwa kinasubili hitma
CCM KIRUMBA KINAWEZA KUWA NA HADHI KWA SIMBA NA YANGA NDIO UWANJA PEKEE WANAOWEZA KUCHEZA BADALA YA TAIFA NA JAMHURI MORO VINGINE INA LILAH LAILA RAJUUN .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers