Nahodha na Mlinda mlango namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania Juma Kaseja
ameshindwa kusaini mkataba na timu ya FC Lupopo ya Congo DRC baada ya
mkataba kuletwa kwa lugha ya Kifaransa.
Kaseja alikubaliana kila kitu na Lupopo ikiwa pamoja na yale aliyotaka yawekwe kwenye mkataba kabla ya kusaini na kwenda kuitumikia klabu hiyo.
Kaseja alikubaliana kila kitu na Lupopo ikiwa pamoja na yale aliyotaka yawekwe kwenye mkataba kabla ya kusaini na kwenda kuitumikia klabu hiyo.
Lupopo wametuma mkataba huo leo lakini imeshindikana kusainiwa kwakuwa
upo kwenye lugha ambayo Kaseja ameomba ibadilishwe na kuwekwa kwenye
lugha ya Kiingereza ili aone kama alichoomba ndicho kilichoandikwa.
Mkataba huo sasa huenda ukasainiwa kesho kama utakuwa umebadilishwa na Kaseja kuridhika na kile kilichomo ndani ya mkataba.
Mkataba huo sasa huenda ukasainiwa kesho kama utakuwa umebadilishwa na Kaseja kuridhika na kile kilichomo ndani ya mkataba.
Kaseja amemaliza mkataba na Simba ambao viongozi wake waliweka wazi kuwa hawataongeza mkataba mwingine na Mlinda mlango huyo aliyedumu zaidi ya miaka 10 kwenye klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment