Usaili
kwa wanaoomba kuteuliwa kuwa wagombea uongozi katika uchaguzi wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na ule wa Bodi wa Ligi Kuu
(TPL Board) unaanza kesho (Agosti 30 mwaka huu).
Kwa
mujibu wa ratiba iliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Agosti 30
mwaka huu ni usaili kwa waombaji uongozi wote katika Bodi ya Ligi Kuu
pamoja na waombaji uongozi wa TFF kwa kanda namba 11 (Morogoro na
Pwani), kanda namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) na kanda namba 13 (Dar es
Salaam).
Agosti
31 mwaka huu ni kanda namba sita (Rukwa na Katavi), kanda namba saba
(Mbeya na Iringa), kanda namba nane (Njombe na Ruvuma), kanda namba tisa
(Lindi na Mtwara) na kanda namba kumi (Dodoma na Singida).
Usaili
kwa kanda namba moja (Geita na Kagera), kanda namba mbili (Mara na
Mwanza), kanda namba tatu (Simiyu na Shinyanga), kanda namba nne (Arusha
na Manyara) kanda namba tano (Kigoma na Tabora), na nafasi za Rais na
Makamu wa Rais wa TFF utafanyika Septemba Mosi mwaka huu.
Waombaji
wote wamepangiwa muda wao wa usaili. Kwa mujibu wa ratiba usaili
ufanyika kuanzia saa 3 kamili asubuhi hadi saa 2 usiku. Wasailiwa wote
wanatakiwa kuzingatia muda waliopangiwa.
No comments:
Post a Comment