HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

10 September 2013

KIPA WA TIMU YA TAIFA APIGWA FAINI

 
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imempiga faini ya sh. milioni moja na kumfungia miezi mitatu Kipa wa zamani wa timu ya taifa na  kocha wa makipa wa timu ya Coastal Union kwa kuwatukana washabiki wanaominika kuwa wa Simba.
Pondamali alifanya kosa hilo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Yanga iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mwamuzi Martin Saanya na mwamuzi msaidizi namba moja Jesse Erasmo waliochezesha mechi kati ya Yanga na Coastal Union nao wamefungiwa mwaka mmoja kila mmoja kwa kutoimudu mechi hiyo.

Nayo Yanga imepigwa faini ya sh. milioni moja (sh. 500,000) kwa kila kosa kutokana na washabiki wake kuwarushia waamuzi chupa za maji baada ya Coastal Union kusawazisha bao katika mechi hiyo. Pia waliwarushia chupa waamuzi hao wakati wakirejea vyumbani baada ya pambano hilo.

Vilevile Coastal Union imepigwa faini ya sh. 100,000 baada ya kuchelewa kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting). Timu hiyo ilichelewa kwa dakika 23. Kikao kinatakiwa kuanza saa 4 kamili asubuhi.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers